Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kwanini Tanzania hatuna Mwamuzi Mkubwa wa kati?

Frank Komba, Mwamuzi Msaidizi.png Frank Komba

Mon, 17 Apr 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Karibu kila nchi Africa ina mwamuzi wake mmoja mkubwa, Tanzania tunaua waamuzi wetu wenyewe.

FRAT, Kamati ya Waamuzi, TFF na wadau tunawajibu mkubwa kuhakikisha tunatengeneza waamuzi wakubwa kama ambavyo tumeshiriki kuwapoteza.

Baadhi ya mifano ya waamuzi wakubwa wa baadhi ya nchi majirani zetu na nyinginezo ni kama hii hapa chini.

1.Rwanda...Samuel Uwikunda

2.Burundi...Pacific Ndabihawehimana

3.Ethiopia...Tessema Bamlak Weyessa

4.DRC ...Ndala Jean-Jaques

5.Somalia ...Hassan Mohamed Hagi

6.South Africa ...Thom Abongile (kabla alikua Victor Gomes ambaye amestaafu)

7.Djibouti...Suleiman Ahmed Djama

8.Mozambique...Celso Alvacao

9.Kenya...Peter Waweru

10.Senegal...Issa Sy na Maguete Ndiaye

11.Zambia (amestaafu mwaka jana Janny Sikazwe)

12.Angola (amestaafu mwaka jana Martins Helder)

13.Botswana...Joshua Bondo

Algeria ...Moustapha Ghobal

14. Gambia …. Bakari Papa Gassama

Tanzania haina hata mwamuzi mmoja wa kati anayecheza level ya Elite matches za Champions League, Shirikisho, wala mashindano yoyote makubwa Afrika. Tuna Frank Komba @kombafrank tu kama mwamuzi msaidizi.

Tuna Ligi namba 5 kwa ubora Afrika, tuna timu 2 kwenye robo fainali ya vilabu Afrika (CAFCL & CC), tunashirikisha timu 4 kwenye mashindano ya vilabu Afrika, hatuna mwamuzi wa kati huko zaidi ya Komba Frank ambaye ni msaidizi.

Tuna shida mahala Tanzania ilikuwa inatoa waamuzi wazuri Afrika na bado uwezo huo tunao.

Tanzania leo ukiambiwa taja Mwamuzi mkubwa na bora wa kati kichwa kuna kuuma.

Hatuwezi kuishi hivyo katika nchi ambako mpira unapendwa kiasi hiki, tuache kurubuni waamuzi wetu tunawapoteza.

Ameandika Jemedari Said

Chanzo: www.tanzaniaweb.live