Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kwani wachezaji wa Simba wanakula nini? - Shabiki

Simba Squad Warm Up.jpeg Kwani wachezaji wa Simba wanakula nini? - Shabiki

Tue, 28 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Shabiki maarufu wa Klabu ya Simba, anayefahamika kwa jina la Mchome amesema kuwa wachezaji wa timu hiyo hiyo hawajitumi uwanjani jambo linalosababisha kupata matokeo mabovu kila mchezo.

Mchome amesema hayo baada ya Simba kuwa na matokeo mabovu ambapo katika mechi tatu za mwisho haijashinda hata mchezo mmoja na ikikumbukwa kuwa imetoka kutoa sare na ASEC Mimosas ya nchini Ivory Coast katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika hatua ya makundi.

"Mechi ya ASEC Mimosas performance ya wachezaji ilikuwa asilimia 5 ya 100, mechi inaanza tu wachezaji wote wamechoka kama wamepuliziwa dawa za kulevya, sijui wanakula nini, uwanjani wanatembea tu, hawajitumi.

"ASEC sio timu ya mpira ni chuo cha mpira, vijana wadogo tu. Timu imecheza hata hatuelewi, Ngoma anacheza namba 10 au beki 3, Saido namba 10 au winga, Che Malone ndiyo haeleweki sijui namba 6.

"Nadhani tatizo la timu viongozi wanajua wenyewe kama ni posho au wachezaji wanadai kwa sababu hakuna kiongozi yeyote aliyetoka akazungumza," amesema mchome.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live