Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kwangu sio mhimu sana kuwajua wachezaji wa Simba - Gamondi

Gamondi Fadlu Debora Kwangu sio mhimu sana kuwajua wachezaji wa Simba - Gamondi

Wed, 7 Aug 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha Mkuu wa Klabu ya Yanga, Miguel Gamondi amesema kuwa sio jambo la msingi sana kwake kuwajua wachezaji wapya wa Simba Sc, badala yake ameelekeza nguvu na akili yake katika kuandaa kikosi chake kufanya vizuri kwenye mchezo wa kesho.

Gamondi amesema hayo leo wakati akizungumza na wanahabari kuelekea mchezo huo wa Nusu Fainali ya Ngao ya Jamii dhidi ya Simba utakaopigwa katika Dimba la Mkapa majira ya saa 1:00.

"Yaliyopita yamepita, ninachokitazama ni mechi ya kesho, siwezo kuhangaika na mambo yaliyopita, huu ni msimu mpya hata Simba wana benchi jipya la ufundi, wachezaji wapya ni tofauti kabisa.

"Tunachokitazama ni kipi kitatokea kesho lakini sisi tumejiandaa na tuko tayari kimwili na kimbinu kuanza msimu mpya, hakiuna jambo jema kama kuanza msimu. Kwetu ni jambo jema kucheza dhidi ya mashabiki wengi na tunaamini uwanja utakuwa full hpouse.

"Kama nilivyosema, Simba wana timu mpya kwa hiyo siwajui vizuri na hasa kwa vile hawajacheza mechi nyingi kama sisi ambavyo tumecheza na za kwetu zilikuwa zinaoneshwa live kwenye TV lakini mwisho wa siku kwangu soka huwa ninawaandaa wachezaji kwa asilimia 70 na asilimia 30 pekee kumfikiria mpinzani.

"Kesho itakuwa mechi ya tofauti labda kwa vile siwajui kivile wachezaji wa Simba lakini kwenye soka hakuna siri na ikizingatiwa ni mechi ya kombe. Kwangu sio jambo la msingi sana kuwajua wachezaji wa Simba. Tutakuja kucheza na kwa uwezo wetu wote na kuhakikisha tunapata ushindi," amesema Gamondi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live