Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kwaheri David De Gea

De Gea David Oo.jpeg David De Gea

Wed, 5 Apr 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

David De Gea ni mmoja ya wachezaji muhimu katika kikosi cha Manchester United hivi sasa, ni 'Legend' wa Manchester United na kwa nafasi yake ameitendea haki jezi ya Manchester United.

Tumtazame De Gea kwanza na falsafa za kocha Erik Ten Hag, vinaenda? bila shaka jibu ni hapana, Ten Hag anataka timu yake ianzishe mashambulizi kutokea nyuma, golikipa awe mtu wa kwanza kupiga pasi, awe na ufundi mguuni, sio tu apige pasi ya mita 5 au 10 kuna nyakati anatakiwa kupiga pasi hata ya mita 60, je hayo De Gea anayaweza?.

Mtazame Allison Becker wa Liverpool, aliwahi kupiga pasi ya mita zaidi ya 50 mpira ukamfikia Salah akaizamisha Manchester United, akarudia tena kupiga pasi ya aina hiyohiyo mpira ukamfikia Salah akaizamisha Manchester City, Allison amekuwa akipiga sana pasi za aina hii ingawa nyingine zimekuwa hazitendewi haki, tofautisha kati ya kupiga pasi na kubutua mbele.

Tumtazame pia Ederson Moraes wa Manchester City, mzuri mguuni, nafikiri linapokuja swala la kufanya saves kwa De Gea wala hakuna mjadala lakini swali ni je? anachokitaka Ten Hag ufanye saves tu? miongoni mwa matukio ambayo nayakumbuka katika mechi za Pre season sauti ya Ten Hag lisikika katika maiki iliyopo karibu nae akishusha tusi baada ya De Gea kubutua mpira bila ya sababu.

Kwa reaction ile tu ilianza kuonyesha nini Ten Hag alikuwa anakitaka kwa kipa wake, je katika umri wake anaweza kubadilika? sidhani, lazima Manchester United wajivike mabomu kuanzia kwa kocha wao, Manchester City waliziba masikio wakaachana na Joe Hart ambae alikuwa ni moja ya makipa bora barani Ulaya.

Liverpool walivunja rekodi ya Dunia kwa upande wa soko la makipa kuinasa saini ya Allison Becker kwa kutoa zaidi ya paundi milioni 60, hawakuangalia tu ni vipi anaweza kudaka anapokuwa langoni, walitaka pia na ufanisi wake anapokuwa na mpira mguuni.

Narejea tena naheshimu kile ambacho David De Gea ameifanyia Manchester United, naheshimu sana uwezo wake lakini kama tunataka kutengeneza muhimili kutokea nyuma its time to say GOODBYE DAVID

Kuna nyakati lazima ujilipue ili kupata mafanikio

Chanzo: www.tanzaniaweb.live