Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kwa wachezji hawa wa Simba, Benchikha atachoka tu - Mchambuzi

Benchikha Mdas Kwa wachezji hawa wa Simba, Benchikha atachoka tu

Wed, 29 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mtangazaji na mchambuzi wa masuala ya soka nchini kupitia EA Radio, Abissay Stephen amesema kuwa Kocha Mkuu mpya wa Klabu ya Simba, Abdelhak Benchikha atachoka tu kuwahamasisha wachezaji wa timu hiyo kwani tatizo kubwa ni uwezo wa wachezaji hao.

Ibra amesema hayo baada ya Simba kumtambulisha Benchikha jana kama kocha wao mkuu baada ya kuachana na Robertinho hivi karibuni.

"Kasi ni adui namba moja wa Simba kwenye kikosi cha sasa, kwa hiyo kusema Benchikha mazoezi yake ya siku chache yataongeza kasi kwa wachezaji ni ngumu kusema hivyo.

"Kusema Benchikha ataongeza fitness ya wachezaji ndani ya hizi siku chache ni ngumu, anaweza kubadilisha mentality, akaongeza kidogo uwezo wa wachezaji kujituma.

"Lakini uwezo wa kujituma wenyewe kuna sehemu utafika utaisha kwa sababu hata ubora wa wachezaji wenyewe umeishia sehemu fulani," amesema Abissay Stephen.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live