Katika mchezo wa Ligi Kuu Bara uliochezwa Uwanja wa Highland Estate ubao umesoma Ihefu 2-1 Yanga baada ya dakika 90.
Ni mabao ya Lenny Kissu dakika ya 40 na lile la ushindi likifungwa na Charles Ilanfya dakika ya 67.
Bao la Yanga limefungwa na Pacome Zouzoua dakika ya 3 ikiwa ni bao la mapema Uwanja wa Highland Estate.
Wachezaji wa Ihefu walikuwa wakipoteza muda hovyo kwa kujiangusha huku Ilanfya akiwa kiongozi wao na alionyeshwa Kadi ya njano, dakika ya 90 ya njano.
Watoa huduma ya kwanza nao mwendo wa kinyonga katika kutoa huduma ya kwanza ilikuwa ni taratibu sana sio sawa. Benchi la ufundi kwa timu zote hakukuwa na utulivu.
Ikumbukwe kwamba dakika 45 za mwanzo kila timu ilionyesha ushindani mkubwa huku timu zikicheza kwa kushambuliana.
Mashabiki wa Yanga nao kipindi cha pili walionekana wakifanya kitendo cha hovyo kwa kurusha chupa uwanjani jambo ambalo sio sawa.