Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kwa sasa Tanzania hakuna klabu inayoifikia Yanga

Hersi Fa835 Eng. Hersi Said.

Tue, 30 Apr 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Raisi wa Klabu ya Yanga SC, Eng. Hersi amesema kuwa kwa sasa hakuna klabu nchini Tanzania ambayo inaweza kufikia ubora wa Yanga.

Yanga ni mabingwa wa watetezi wa Ligi Kuu ya NBC, ubingwa ambao wameuchukua mara mbili mfululizo na yupo mbioni kutwaa tena Ubingwa huo huku akiwa amecheza fainali ya CAFCC na kuingia robo fainali ya CAFCL.

"Kwa sasa hakuna Klabu Tanzania inayoweza kuisogelea Young Africans SC kwenye ubora. Ndio maana timu nyingi zikicheza na sisi zinakuja na mfumo wa kuzuia zaidi ikimaanisha wanaiheshimu Klabu yetu. Malengo yangu makubwa ni kuhakikisha Klabu yetu inakuwa moja ya Klabu bora Afrika.

"Na matamanio yangu ni kuona mwakani kwenye mashindano ya Kimataifa tufike katika orodha ya timu nne bora AFRIKA, ili tuweze kushiriki Kombe la Dunia la Vilabu. Mwaka jana tumefika fainali na tumepata alama nyingi ambazo zitatuongezea nguvu ya kushiriki Kombe hilo," amesema Eng. Hersi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live