Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kwa rekodi hizi za Yanga, Geita Gold wajiandaandae kwa 5G?

Yanga Tano Pacome Maxi 191929 Kwa rekodi hizi za Yanga, Geita Gold wajiandaandae kwa 5G?

Thu, 14 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Ni siku nyingine tena leo timu ya Young Africans SC inashuka dimbani kuwania pointi tatu dhidi ya Geita Gold.

Mchezo huo wa Ligi Kuu ya NBC, utachezwa Uwanja wa Azam Complex uliopo Chamazi, Dar es Salaam kuanzia saa 2:15 usiku.

Kocha Mkuu wa Young Africans SC, Miguel Gamondi, amesema ni muhimu kuendelea kupata pointi tatu katika mechi zote zilizosalia ili kutetea taji letu la Ligi Kuu ya NBC ambapo mpaka sasa tumecheza mechi 18 na kukusanya pointi 49 zinazotufanya kuendelea kusalia kileleni mwa msimamo.

Katika mchezo wa mzunguko wa kwanza wakiwa ugenini, waliifunga Geita Gold magoli 3-0, wafungaji wakiwa ni Pacome Zouzoua, Stephane Aziz Ki na Maxi Nzengeli.

Rekodi zinaonesha kwamba, tangu mwaka 2021, Yanga imekutana na Geita Gold katika michezo mitano ya Ligi Kuu ambayo yote tumeshinda.

Geita Gold hawajawahi kupata ushindi dhidi yetu, ambapo katika mechi hizo tano, tumefunga magoli 9 na kuruhusu 1, huku wakikusanya clean sheets 4.

Matokeo yapo hivi;

Oktoba 2, 2021 (Yanga 1-0 Geita),

Machi 6, 2022 (Geita 0-1 Yanga),

Oktoba 29, 2022 (Geita 0-1 Yanga),

Machi 12, 2023 (Yanga 3-1 Geita) na

Oktoba 7, 2023 (Geita 0-3 Yanga).

Yanga msimu huu imekuwa ya moto ikiwa inaongoza ligi mpaka sasa baada kucheza michezo 18 na kufunga mabao 47 ikiruhusu mabao 9 pekee.

Aidha, yanga imezifunga timu nane mabao matano matano kwenye mchezo mmoja mmoja wakiwemo wapinzani wao Yanga, na mchezo uliopita wametoka kumfunga Ihefu bao 5-0 baada ya kuwasumbua misimu miwili.

Yanga imetangaza kiingilio cha mechi hiyo kuwa ni Tsh 20,000 Jukwaa la V.I.P A, Tsh 10,000 V.I.P B na Tsh 5,000 Mzunguko, utaushuhudia mchezo huu, hivyo fanya haraka kununua tiketi yako mapema ili twende uwanjani kuisapoti timu yetu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: