Ikiwa utapata muda wa kuwahukumu wale wabaya wako basi hautapata muda wa kuwapenda ila ukiwafikiria kuwabadilisha utakuwa kwenye ulimwengu wako. Sasa kuna miamba ambayo ukifikiria kuhusu mabao huwezi kuiweka kando wanajua kufunga na wana hat trick zao, hapa tupo nao kwenye mwendo wa data namna hii;
JOHN BOCCO Huyu ni kinara wa kutupia hat trick ndani ya Ligi Kuu bara akiwa nazo mbili na katupia jumla ya mabao tisa na pasi moja ya bao.
Ni kwenye mchezo dhidi ya Ruvu Shooting alitupia dakika ya 4, 17 na 68 ilikuwa Uwanja wa Mkapa Novemba 19, 2022 ambapo mabao yote alifunga akiwa ndani ya 18 akitumia mguu wa kulia.
Katika mchezo huo Simba ilishinda kwa mabao 4-0 dhidi ya Ruvu Shooting na kusepa na pointi tatu mazima.
Timu ya pili ni Tanzania Prisons ambapo alifunga dakika ya 12, 46 na 62 ilikuwa Uwanja wa Mkapa yote akiwa ndani ya 18.
SAIDI NTIBANZOKIZA ‘SAIDO’ Ni ingizo jipya ndani ya Simba likiwa limeanza kwa kasi kwenye mchezo wake wa kwanza aliweka rekodi ya kuwa nyota aliyefunga hat trick msimu huu baada ya kuibuka hapo akitokea Geita Gold.
Ilikuwa dakika ya 60, 64 na 69, wakati ubao wa Uwanja wa Mkapa ukisoma Simba 7-1 Tanzania Prisons ilikuwa Desemba 30, 2022 na alifunga mabao yote hayo akiwa ndani ya 18.
JEAN BALEKE Ingizo jipya lingine ndani ya Simba lina jumla ya mabao matano kwenye ligi huku likiwa limewaka kwenye upande wa kucheka na nyavu.
Anakuwa staa wa kwanza kutoka ndani ya Simba na Yanga kufunga hat trick yake nje ya Dar ambapo ni kwenye Uwanja wa Manungu.
Baleke alifunga wakati ubao wa ukisoma Mtibwa Sugar 0-3 Simba alifanya hivyo dakika ya 3,8 na 34 wakati Simba ikisepa na pointi tatu mazima ugenini ilikuwa ni Machi 11,2023.
Inakuwa ni hat trick ya kwanza ndani ya 2023 baada ya mwaka 2022 kugota ukingoni ukurasa ndiyo kwanza unafunguliwa.
FISTON MAYELE Ukimuona tu unajua kazi tunayo kwa kuwa anapenda kufunga na uwezo anao na nia anayo popote yeye anatupia kitaifa na kimataifa anaitwa Mayele ni mali ya Yanga. Nyota wa kwanza kufunga hat trick msimu wa 2022/23, alifanya hivyo kwenye mchezo dhidi ya Singida Big Stars walipowatungua 4-1.
Mayele alifanya hivyo dakika ya 26,15 na 55. Mayele ni mwamba pekee mwenye bao kwenye hat trick akiwa nje ya 18, ilikuwa dakika ya 26 huku yale mawili mengine akitupia akiwa ndani ya 18 ilikuwa Novemba 17, 2022.
SAIDO KAWAFUNIKA WOTE Nyota Saido licha ya kuwa na hat trick moja kibindoni kawafunika wote kwa kuwa amefunga hat trick ya mapema zaidi ndani ya dakika 10, kazi alimaliza na kuweka rekodi yake ambayo bado haijavunjwa na wanaofuata kwa msimu huu.
Vinara wa mabao Ligi Kuu Tanzania Bara (NBC Premier League)
1. Fiston Mayele (Yanga) - 15 2. Moses Phiri (Simba) - 10 3. Said Ntibazonkiza (Geita/Simba) - 10 4. Bruno Gomez (Singida) - 9 5. John Bocco (Simba) - 9 6. Sixtus Sabilo (Mbeya City) - 9.
NBC PL 22/23 mapaka sasa.
✅ Most Goals (Simba): 58 ✅ Most shots on Target (Simba): 142 ✅ Top Scorers -Mayele: 15 -Saido: 10 -Phiri: 10 -Bocco: 9
✅ Top Assists -Chama: 14 -Saido: 9.
Magoli ya mapema zaidi mpaka Sasa ligi kuu Msimu wa 2022/23. 1. Prince dube Vs Simba sec 15 2. Kibabage Vs Mbeya City sec 58 3. Ismail mgunda Vs Dodoma dk 1 3. Moses Phiri Vs KMC dk 2 5. Ally kipemba vs KMC dk 3 6. Matheo Anthony Vs ihefu dk 3.