Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kwa ratiba hii, timu hizi zitapigwa sana

Simba Yanga Mzmzm Kwa ratiba hii, timu hizi zitapigwa sana

Thu, 15 Aug 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Msimu mpya wa 2024-2025 wa Ligi Kuu Bara unaanza rasmi Agosti 16 huku ukiratajiwa kuhitimishwa Mei 24, mwakani ingawa moja ya kilio kikubwa kwa makocha wengi wa timu shiriki ni kutopenda kucheza michezo ya mchana kutokana na jua kali.

Wakati ratiba ya msimu huu ikiwekwa wazi, zipo timu ambazo zitakuwa na kazi kubwa ya kufanya kwani asilimia kubwa ya michezo yao itacheza katika kipindi cha jua kali kali, kwa maana ya saa 8:00 za mchana kama Mwanaspoti linavyozielezea.

TABORA UNITED Ratiba ya awali inaonyesha Tabora United ndiyo ambayo itakuwa na wakati mgumu zaidi wa kucheza katika kipindi cha jua kali kwa maana ya saa 8:00 za mchana kwa sababu itakuwa na jumla ya michezo 11 kati ya 30 itakayoicheza kwa muda huo.

Michezo ya Tabora United ni na Kagera Sugar (Septemba 11), KenGold (Septemba 28), Pamba (Novemba 2), KMC (Novemba 29), Namungo FC (Desemba 28), Fountain Gate (Februari 1, 2025), TZ Prisons (Februari 15, 2025) na Dodoma Jiji ((Februari 22, 2025).

Mingine ni dhidi ya Pamba Jiji (Machi 29, 2025), Mashujaa (Aprili 13, 2025) huku wa mwisho ni na KMC utakaopigwa Mei 4, 2025.

KENGOLD Timu hii ambayo imepanda Ligi Kuu Bara msimu huu, ratiba inaonyesha itakuwa na michezo minane ambayo itachezwa saa 8:00 za mchana, ikiwa ni sawa pia na kikosi cha Maafande wa Tanzania Prisons ambazo zote zinapatikana katika Jiji la Mbeya.

Michezo ya KenGold ni dhidi ya Singida Black Stars (Agosti 18), Tabora United (Septemba 28), JKT Tanzania (Oktoba 4), Coastal Union (Novemba 23), Namungo FC (Desemba 16), Fountain Gate (Januari 20, 2025) na KMC (Februari 16, 2025).

Wa mwisho ni dhidi ya Tanzania Prisons (Aprili 11, 2025), huku kwa upande wa michezo ya Tanzania Prisons ni Dodoma Jiji (Septemba 21), Singida Black Stars (Desemba 15), Pamba Jiji (Desemba 20), Namungo FC (Januari 26, 2025) na Tabora United Februari 15, 2025).

Mingine ni Fountain Gate (Februari 21, 2025), Kagera Sugar (Machi 30, 2025) huku mchezo wa mwisho ni na KenGold (Aprili 11, 2025).

PAMBA JIJI Timu zinazofuata ambazo zitacheza mchana kweupe, ukiachana na Tabora United, KenGold na Tanzania Prisons, nyingine ni Dodoma Jiji, Singida Black Stars na wageni wa Ligi Kuu Bara msimu huu Pamba ambapo zitakuwa na michezo mitano kila mmoja wao.

Michezo ya Pamba ni dhidi ya Singida Black Stars (Septemba 15), Tabora United (Novemba 2), Tanzania Prisons (Desemba 20), Namungo FC (Machi 9, 2025) na Tabora United (Machi 29, 2025), huku Singida Black Stars ikianza na KenGold (Agosti 18).

Baada ya hapo itacheza na Pamba (Septemba 15), Dodoma Jiji (Desemba 12), Tanzania Prisons (Desemba 15) na JKT Tanzania (Januari 24, 2025), huku Dodoma Jiji ikianza na Tanzania Prisons (Septemba 21), Coastal Union (Oktoba 18) na Singida BS (Desemba 12).

Michezo mingine ya Dodoma Jiji ni dhidi ya Tabora United (Februari 22, 2025) na kuhitimisha mbele ya JKT Tanzania (Machi 8, 2025).

KMC Timu hii itakuwa na michezo minne ya mapema kama ilivyokuwa pia kwa Coastal Union, Fountain Gate, Namungo FC na JKT Tanzania.

Michezo ya KMC ni dhidi ya Tabora United (Novemba 29), KenGold (Februari 16, 2025), Fountain Gate (Februari 28, 2025) na Tabora United (Mei 4, 2025), huku ya Coastal Union ni JKT Tanzania (Septemba 25), Dodoma Jiji (Oktoba 18) na KenGold (Novemba 23).

Mchezo wa mwisho wa mapema kwa Coastal ni na Mashujaa (Januari 19, 2025) huku ya Fountain ni dhidi ya KenGold (Januari 20, 2025), Tabora United (Februari 1, 2025), Tanzania Prisons (Februari 21, 2025) kisha kuhitimisha na KMC (Februari 28, 2025).

Kwa upande wa Namungo ni dhidi ya KenGold (Desemba 16), Tabora United (Desemba 28), Tanzania Prisons (Januari 26, 2025) na Pamba (Machi 9, 2025), huku JKT Tanzania ikiwa na Coastal Union (Septemba 25), KenGold (Oktoba 4), Singida Black Star Januari 24, 2025).

Mchezo wa mwisho wa mapema kwa Maafande hao wa JKT Tanzania, utakuwa ni dhidi ya Dodoma Jiji ambao utapigwa Machi 8, 2025.

MASHUJAA Timu za Mashujaa ya Kigoma na Kagera Sugar ya Bukoba, zitakuwa na michezo mitatu tu ambayo itachezwa mapema saa 8:00 za mchana.

Michezo ya Mashujaa ni dhidi ya Kagera Sugar (Novemba 30), Coastal Union (Januari 19, 2025) na Tabora United (Aprili 13, 2025), huku Kagera Sugar ikianza na Tabora United (Septemba 11), Mashujaa (Novemba 30) kisha Tanzania Prisons (Machi 30, 2025).

MSIKIE FIKIRI Kocha Mkuu wa KenGold, Fikiri Elias anasema, japo kwa kiasi kikubwa inaumiza kutokana na michezo hiyo mingi kuchezwa kwa muda huo, hana kisingizio ila anachofanya ni kuiandaa timu itakayompambania kupata matokeo bora katika mazingira yoyote.

“Sio mara ya kwanza kwa sababu hata wakati timu inashiriki Ligi ya Championship imeshacheza michezo mingi ya mapema na bado ikaendelea kupata matokeo mazuri, sisi kama benchi la ufundi na wachezaji tumejipanga kwa namna yoyote,” anasema.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live