Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kwa nini wachezaji wa nje wameongezeka Tanzania?

Mastaa Yanga Ubingwa Kwa nini wachezaji wa nje wameongezeka Tanzania?

Mon, 26 Jun 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wachezaji wa kigeni wana faida na hasara zake, Rais Mstaafu Mh. Dkt. Jakaya Kikwete juzi wakati anafunga mashindano ya JKT Marathon aligusia kuhusu kufanya tathmini ya idadi ya wachezaji wa kigeni kwa sababu awali klabu moja iliruhusiwa kusajili wachezaji nane lakini sasa hivi imeongezeka na kufikia 12!

Timu zetu zinapata mafanikio, watanzania wangapi ni sehemu ya hayo mafanikio? Mfumo wa soka letu umejengwaje kwa ajili ya kuzalisha wachezaji ili waingie kwenye soko la ushindani?

KWA NINI WACHEZAJI WA KIGENI WAMEONGEZEKA?

Klabu hizi kubwa ambazo zinashiriki mara kwa mara mashindano ya kimataifa baada ya kuona haziwezi kushindana na klabu nyingine kubwa kwa sababu vikosi vyao vinaundwa na wachezaji bora kutoka mataifa tofauti, klabu zetu zikaomba kuongezewa idadi ya kusajili wachezaji wa kimataifa.

Kwa kuwa lengo lao lilikuwa ni kufanya vizuri kwenye mashindano ya kimataifa na kufikia malengo, zikaruhusiwa kusajili hadi wachezaji 12 na kuwatumia wote kwa pamoja.

Baada ya kuruhusiwa kusajili wachezaji wengi raia wa kigeni, klabu zetu zimethibitisha ubora wao kwenye mashindano ya kimataifa. Simba imecheza Robo Fainali nne za mashindano ya CAF, msimu huu Yanga imeenda hadi Fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika.

Ukweli usiopingika ni kwamba, wachezaji wengi waliosaidia mafanikio hayo ni wachezaji wa kigeni.

Rais Mstaafu wa awamu ya nne Mh. Jakaya Kikwete aligusia kuwa, hawa wachezaji wengi wa kigeni wanaoendelea kuja nchini wanasaidiaje maendeleo ya mpira wa miguu nchini? Nafasi ya wachezaji wazawa ipoje?

Ni ukweli kuwa wachezaji wengi wanaong’aa nchini ni wageni, wanang’aa kwa sababu wanapata nafasi ya kucheza mara kwa mara.

USHAURI WANGU

Pamoja na kwamba tunataka kushindana kwenye soka la kimataifa, tunahitaji kuwa na idadi fulani ya wachezaji wa kigeni lakini tuwekeze kwenye kuzalisha wachezaji wetu.

Tuwaandae vijana wetu katika misingi ambayo itawafanya wawe bora na weweze kushindana kwenye soko la ushindani.

Tusizalishe wachezaji ambao tutawatafutia nafasi, kwamba tulazimishe wazawa wawepo kwenye timu hata kama hawana uwezo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: