Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kwa nini majeruhi wa Simba wanachelewa kupona?

Aubin Kramo Manula Kwa nini majeruhi wa Simba wanachelewa kupona?

Wed, 17 Apr 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kiungo Aubin Kramo alikuwa bora sana wakati anatoka kwenye Klabu ya ASEC Mimosas, lakini tangu apatwe na majeraha pamoja na kushindwa kudeliver akiwa Msimbazi, anaungana na nyota wengi bora waliotoka kwao wakiwa bora ila wakadrop wakiwa Simba.

Mtazame Jean Baleke nyakati za mwisho alishaanza kupoteza makali yake, mkumbuke hata Pape Ousmane Sakho alishaanza kupoteza makali yake mwishoni, Peter Banda alikuwa na majeraha mengi na akashindwa kuperform, Moses Phiri, Aishi Manula hajulikani hata alipo kwa sasa.

Talented Boy kama Augustine Okrah nae alianza kudrop siku hadi siku tofauti na alivyokuja na akaondoka kwa kigezo cha mambo ya nje ya uwanja ila kwa sasa anauwasha ndani ya Yanga na husikii mambo ya nje ya uwanja, Jonas Mkude ni kama amezaliwa upya Jangwani na anaonesha.

Kwa nini?

Mchezaji anayekaa benchi Simba akipewa nafasi ya kucheza huoni akikupa mechi bora tofauti na aliyempisha. Lakini ukienda Jangwani, mchezaji anayeketi benchi hata mechi 10+ bado akiingia atadeliver kwa ubora mkubwa.

Kuna maswali mengi hapa?

Mudathir Yahya katoka kukaa nje kwa muda mrefu sana halafu anaenda kuuwasha tena ndani ya Yanga, hili linafikirisha sana! Sureboy alitoka Azam anaenda Yanga ni kama kashusha umri wake, Khalid Aucho katoka majeruhi ni kama hakuwahi kuumia, Jesus Moloko aliwahi kuumia akafanyiwa upasuaji akarejea fiti, unamkubuka Yakouba Sogne?

Kibwana Shomari si mara ya kuumia tena vibaya sana, lakini akirejea anaushawa ileile. Lomalisa aliumia hivi karibuni mechi dhidi Al Ahly, lakini leo ni kama alikuwa fiti tangu msimu uanze, Farid Musa, Zawadi Mauya na wengine wengi.

Maswali ya kujiuliza ni kama yafuatayo.

1. Kwa nini kuna changamoto za majeraha sana ndani ya Simba? Na mchezaji akirejea sio yule tena.

2. Kwanini wachezaji wengi wakija Simba na ubora wao, wengi wanaondoka wakiwa wamefeli kabisa?

3. Mchezaji akikaa benchi Simba bila kucheza, akipewa nafasi ni kama hakuwahi kucheza mpira maishani mwake?

Hili suala linaumiza sana kichwa wana Msimbazi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live