Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kwa nini lawama zote kwa Bocco?

Bocco Vs Raja John Bocco

Sat, 25 Feb 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Nimeona kwa sasa lawama nyingi zimekuwa kwenye safu ya ushambuliaji ya Simba kitaifa na kimataifa, hakika ni kweli wanakosea na wanashindwa kufunga lakini je lawama hizi zinamstahili John Bocco pekee?

Ukianza kwenye mechi za ligi ule dhidi ya Azam FC wakati wakitoshana nguvu kwa kufungana bao 1-1 bado Bocco anatajwa kuwa sababu za Simba kushindwa kupata ushindi.

Mjadala mkubwa umekuwa ni namna anavyopokea pasi na kuzipoteza akiwa ndani ya 18 hilo ni sawa lakini je mnasahau kwamba hata yeye kwenye mchezo huo alitengeneza nafasi moja ya wazi ambayo hakuna mchezaji wa Simba aliyefanikiwa kuibadili kuwa bao?

Kwenye anga za kimataifa dakika 180 Simba imeshindwa kufunga ni kweli lakini ni Bocco peke yake ambaye alifanya makosa ya kushindwa kufunga?

Katika muda aliopewa mnasahau kuwa kuna wakati aliokoa hatari licha ya kuwa ni mshambuliaji na kuliweka lango la Air Manula salama.

Mijadala imekuwa mingi naona inamuangalia Bocco kama tatizo na kusahau kwamba kushinda ni kwa timu na kushindwa kunaihusu timu.

Moja ya wazawa wanaofanya kazi kubwa wanapopewa nafasi je afanye nini kwa sasa anapopewa zigo la lawama peke yake akiwa ni nahodha?

Kwenye mtandao wakati Simba wameachia posti ya mazoezi ya Simba kuna mdau akauliza ‘Bocco anapasha ili iweje?

Hakika anastahili kuambiwa aongeze umakini lakini sio kwa kiwango hiki.Benchi la ufundi limeweka wazi kuwa kwenye kila mchezo nafasi zinatengenezwa lakini kuzibadili kuwa mabao hapo ndio tatizo.

Muhimu kila mmoja ndani ya Simba kutimiza majukumu yake lakini lawama zisianguke kwa mchezaji mmoja tuna amini Bocco anapenda kufunga inatokea bahati mbaya, wakati unakuja atafanya kazi nzuri.

Kutofunga kwenye mechi mbili za kimataifa kunaumiza lakini kumpa zigo mchezaji mmoja kunaumiza zaidi. Kila la kheri Simba kwenye mchezo wenu dhidi ya Vipers, safu ya ushambuliaji tunaamini itakuwa na kitu cha tofauti wakati huu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live