Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kwa nini kila mtu anataka kujenga fremu? - Makonda

Makonda Aeleza Ramani Ya Kazi Arusha Paul Makonda.

Mon, 22 Apr 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mkuu wa Mkoa wa Arusha amehoji sababu zinazofanya kila mtu jijini Arusha kufikiria au kujenga fremu za maduka wakati uhitaji mkubwa kwenye jiji hilo ni vyumba vya kulala?

Makonda amesema wananchi wa Arusha wanatakiwa kubadilika na kuona kwamba ujenzi wa nyumba au vyumba vya kulala ndiyo uhitaji mkubwa kutokana na jiji hilo kuwa na wageni wengi wakiwemo watalii.

Amesema kiwango cha fedha anachoweza kupata mtu aliyejenga vyumba vya kisasa vya kulala ni kikubwa kuliko anachokipata mtu aliyejenga fremu.

Makonda ameyasema hayo wakati akizungumza na watumishi wa Jiji la Arusha kwenye Kituo cha Mikutano ya Kimataifa Arusha - AICC Ukumbi wa Simba jana Aprili 21, 2024.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live