Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kwa nini hatumzungumzi Bakari Shime?

Shime Jkt Rf.png Kwa nini hatumzungumzi Bakari Shime?

Mon, 11 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Yani tunafanya makusudi. Ila ukweli ni hatumpi Bakari Shime sifa anazostahili. Amebadili kabisa taswira ya timu za taifa za wanawake nchini. Ameweka heshima kubwa katika eneo hilo.

Ni majuzi tu ametupeleka Fainali za Afrika kwa Wanawake zitakazofanyika mwakani Morocco. Ni fahari kubwa sana.

Huwa inatokea mara chache kwa nchi kama Tanzania kufuzu katika fainali hizo. Tulikua nyuma sana katika soka la wanawake wakati Shime anachukua timu miaka kadhaa nyuma.

Akaanza kutengeneza ufalme kwenye Ukanda wa CECAFA. Tukatwaa mataji kadhaa ya ukanda wetu.

Kisha timu ikaanza kushiriki mashindano ya Kusini mwa Afrika (COSAFA). Tukaweka utawala wetu katika ukanda huo. Tukatwaa mataji kadhaa kuanzia ngazi za vijana hadi wakubwa.

Kule COSAFA timu za Taifa za Wanawake zina heshima kubwa sana.

Kisha akaipeleka Serengeti Girls kwenye Fainali za Kombe la Dunia pale India. Ni historia kubwa sana. Kisha timu ikafika Robo Fainali ya mashindano.

Huyu ndiye Bakar Shime, kocha mzawa aliyebadili kila kitu upande wa soka la wanawake. Kwa nini hatumpatii sifa anazostahili? Sijui.

Ila hizi sifa wanazopewa kina Miguel Gamondi na Benchikha alistahili pia kupewa Shime. Amefanya kazi kubwa sana.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live