Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kwa nini Yanga wanakwepa kudai fidia kwa Fei Toto? - Jemedari

JEMEDARI.png Jemedari Said

Sun, 7 May 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kwa nini Yanga wanakwepa kudai fidia kwa mchezaji ambaye ameonyesha nia na amevunja mkataba?

Mchezaji ambaye ameandika barua kwa klabu, ameandika barua kwa TFF kuomba kuvunja mkataba, hakuna kipengele cha fidia kwenye mkataba wake? Jibu kipengele kipo, ambacho ni 17.4.

Mchezaji haitaki klabu na klabu inamng’ang’ania unajiuliza kwanini? Kama Yanga wangeamua kuvunja mkataba na kumwambia mchezaji hatukutaki kama Fei alivyoiambia Yanga, wao Yanga wasingemlipa fidia kutoka kwenye mkataba baina yao?

Kamati mara 3 inasikiliza shauri hili na kusema FEISAL amekosea, ok baada ya kukosea adhabu gani anapewa mkosefu huyu?

Au hiyo kurudishwa Yanga ndiyo adhabu yake? Kwanini kamati inakwepa kumuadhibu Feisal kwa makosa yake na badala yake inamlazimisha kurudi mahala alikosema hataki na akaamua kuvunja mkataba nao? Kwani wachezaji wamekuwa watumwa sasa hivi wa kulazimishwa kukaa mahala wasipopataka?

Kuna sehemu kuna shida lazima, hizi kamati za sheria zinafaa kuundwa na wanasheria tena wasiokuwa na maslahi na vilabu, panapotokea mgongano wa maslahi waeleze wazi na wajitenge na hilo shauri sio kama ilivyo sasa.

Rais wa TFF ambaye huteua wajumbe wa hizi kamati anapaswa kuliona hili na kulifanyia kazi. Kamati hii ya sheria na hadhi Ina wajumbe 7 ndani yao wanasheria ni 2 tu Alex Mgongolwa (Makamu Mwenyekiti) na Hussein Kita, wajumbe wengine 5 sio wanasheria akiwemo na Mwenyekiti MZEE Said Sudi. Ingawa kanuni inaruhusu hili kutokea lakini busara na maarifa kwa mamlaka ya uteuzi inafaa kutumika.

Shauri hili liko wazi kabisa kuna shida za kimgongano wa maslahi na siasa za mpira ndiyo zinakwamisha Feisal kupewa haki yake hata ya kutozwa faini au kulipa fidia kwakuwa wanajua hiyo maana yake nini.

BIN KAZUMARI MTIPA (The voice of the voiceless)

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: