Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kwa nini Yanga wamefanya kiingilio bure?

Mashabiki Wa Yangaa Mashabiki wa Yanga.

Mon, 18 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mchambuzi wa masuala ya soka nchini kutoka Sport Extra ya Clouds FM, James Tupatupa amefunguka kuhusu Klabu ya Yanga kuamua mashabiki zake waingie bure kwenye mchezo wao wa marudiano wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Medeama FC.

Katika mchezo huo utakaopigwa Jumatano, Desemba 20, 2023 katika Dimba la Mkapa, mfadhili wa Yanga, Ghalib Said Mohammed amenunua tiketi zote za jukwaa la mzunguko, hivyo mashabiki wataingia bure.

“Mechi dhidi ya Medeama sio mechi ya kwanza kwenye hatua ya makundi kwa Yanga, kwa mechi za nyumbani hii ni mechi ya pili, kwa hiyo inategemea mechi iliyopita wameona nini.

“Mechi iliyopita ilikuwa na kiingilio inawezekana waliona hadi dakika ya mwisho kuna kusuasua basi safari hii wamenunua, lakini pia wanaangalia trend ya mashabiki kuingia uwanjani.

“Tangu msimu huu umeanza kwenye Tamasha la Yanga Day wanaangalia je namba ya watu inakuwa kubwa au inakuwa ndogo? kama ni kubwa vizuri ila kama ni ndogo hatutaki picha yenye mapengo. Mwisho wa siku lazima uingie mfukoni,“ amesema Tupatupa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live