Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kwa nini Yanga kuwania Tuzo ya Klabu Bora Afrika?

Yanga Zali Kwa nini Yanga kuwania Tuzo ya Klabu Bora Afrika?

Fri, 3 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mchezaji wa zamani wa Simba na Yanga pamoja na timu ya Taifa ya Tanzania, Amri Kiemba amesema kuwa daraja la timu kwenye orodha ya timu Bora Afrika huwekwa kutokana na alama ambazo timu husika inakuwa imekusanya ndani ya misimu kadhaa.

Kiemba amesema hayo wakati akifafanua kuhusu ubora dhidi ya kiwango cha timu baada ya Klabu ya Yanga kuchaguliwa miongoni mwa timu 10 Afrika zinazowania Tuzo ya Klabu Bora ya Mwaka ya CAF wakati wapinzani wao Simba wakiwa hawamo kwenye orodha hiyo.

"Ranks za ubora wa klabu hutokana na daraja ambalo klabu imeweka kwa kukusanya points sio kiwango ndani ya msimu fulani!

"Marumo Gallants msimu uliopita ilikuwa na kiwango bora kwenye Kombe la Shirikisho Afrika, tunavyozungumza Marumo imeshuka daraja kutoka Ligi Kuu ya Afrika Kusini.

"Kwenye ranks za ubora timu haiwezi kuingia kwa hamasa wala maneno matupu, zile sio kama tuzo watu wanaamua wampe nani!," amesema Amri Kiemba.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live