Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kwa nini Uwanja wa Mkapa unafanyiwaukarabati?

Eze Kamwaga Ezekiel Kamwaga

Sun, 30 Jul 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Juzi Serikali ilitoa taarifa kuwa Uwanja wa Benjamin Mkapaunakwenda kufanyiwa ukarabati kwa Gharama ya Tsh. Bilioni 31.

Sasa Mwandishi wa Habari Mkongwe nchini Ezekiel Kamwaga amekuja na hojakufafanua ukakasi juu ya Gharama za ukarabati wa Uwanja huo wa Benjamin Mkapa.

Wapo wadau waliohoji iweje uwanja uliogharimu shilingi bilioni 50, ukarabati wake uwe shilingi bilioni 31? Kwanza, wakati uwanja unakamilika mwaka 2007, gharama ilikuwa dola milioni 56 za Marekani (sio bilioni 50 zinazosemwa).

Hii maana yake ni kwamba, kama uwanja huu ungekuwa umejengwa mwaka huu, gharama yake ingekuwa takribani shilingi bilioni 137 za Tanzania. Kwa viwango hivyo vya mwaka 2007, marekebisho haya ya sasa ni sawa na shilingi bilioni 20.4. Hivyo, gharama ya uwanja huu kwa sasa inatakiwa iwe shilingi bilioni 137 kwa thamani ya dola ya wakati huu.

Kimsingi, kwa sasa gharama zilizo kwenye mitandao kwa nchi zinazotaka kujenga uwanja wa aina ya Benjamin Mkapa zinakadiriwa kuwa kati ya dola milioni 100 hadi milioni 160 (kati ya shilingi bilioni 240 hadi bilioni 350).

Mfano wa ukarabati wa viwanja ni Uwanja wa Amaan, Zanzibar. Uwanja huo sasa unafanyiwa marekebisho makubwa utakaowezesha kuwa na uwezo wa kuingiza washabiki takribani 15,000. Kwa mujibu wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), kiasi cha shilingi bilioni 15 zitatumika kwa ukarabati huo.

Uwanja wa Mkapa unaingiza watazamani mara nne ya uwanja huo wa Amaan lakini gharama za marekebisho ni takribani mara mbili tu ya uwanja huo wa Zanzibar.

Mimi ni shabiki wa Liverpool ya Uingereza. Mwaka 2021, klabu iliamua kuongeza uwezo wa uwanja wa Anfield kuingiza washabiki kutoka 53,000 hadi 61,000 (sawa na kwa Mkapa). Gharama za marekebisho ya jukwaa litakalohusika, lile la Anfield Road Stand, imekadiriwa kufikia dola milioni 97 (sawa na takribani shilingi bilioni 237 za Tanzania).

Haya ni marekebisho yanayohusu upande mmoja tu wa jukwaa kwa kuongeza viti 8,000.

Kwa hiyo gharama hizi za ukarabati wa uwanja zinaendana na gharama za marekebisho makubwa yanayofanyika katika viwanja vingine duniani.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live