Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kwa nini Saido anachukiwa?

Saido Ntibazonkizaaaaaaaaaaa Kwa nini Saido anachukiwa?

Thu, 6 Jun 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kwenye funga kazi ya msimu wa 2023/24 ndani ya kikosi cha Simba kinachonolewa na Kocha Mkuu Juma Mgunda mwamba wa kazi Saido Ntibanzokiza alikiwasha.

Pengine kazi yake ingekuwa hivyo tangu mwanzo wa msimu alikuwa na nafasi ya kuvunja rekodi yake ya msimu wa 2022/23 kwa kutupia mabao 17 lakini upepo ulikuwa tofauti.

Kiungo mshambuliaji wa Simba kasi yake kwenye mechi tatu za mwisho ilikuwa ni moto. Alifunga mabao mawili kwenye mchezo dhidi ya Geita Gold, bao moja dhidi ya KMC na bao moja dhidi ya JKT Tanzania. Ndani ya dakika 270 alitupia mabao manne.

Ni namba moja kwa mastaa wenye mabao mengi ya penalti ambayo ni saba akiwa ni namba moja kwa utupiaji kikosi cha Simba ambapo jumla kafunga mabao 10 na mguu wake wenye nguvu ni ule wa kulia.

Inaelezwa kuwa huenda akasepa ndani ya kikosi cha Simba kwa ajili ya kupata changamoto mpya katika timu nyingine tofauti na Simba.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live