Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kwa nini Paul Pogba hatakiwi Barcelona?

Paul Pogba A 1536x864 Kiungo wa Manchester United, Paul Pogba

Wed, 15 Dec 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Taarifa za chini ya kapeti zinadai kuwa raisi wa Barcelona, Joan Laporta amekataa kumsajili nyota wa Mashetani Wekundu, Paul Pogba baada katika mazungumzo yake na wakala wa nyota huyo.

Wakala Mino Raniola na Joan Laporta wanaripotiwa kuwa walipata fursa ya kuonana Jumaane, na wakafanya mazungumzo juu ya biashara za majina kadhaa ya wachezaji, Jina la Paul Pogba pia liliibuka kwenye mazungumzo yao.

Nyota huyo wa Ufaransa anatazamia kuwa mchezaji huru msimu ujao wa joto, wakati mkataba wake wa sasa ukiwa ukingoni.

Licha ya ugumu wa swali la uwezo wa Barcelona kufikia gharama ya mshahara wa Paul Pogba, Barca wanaonekana kuwa hawana kabisa mpango naye.

Kwa mujibu wa chapisho la kihispania la Sport Laporta ametajwa kuwa amemwambia Mino Raniola kuwa Paul Pogba hatakiwi Camp Nou.

Sababu kubwa inayotajwa ni kuwa Barca hawaoni kama anafaa kwenye aina ya kiungo ambaye kocha mkuu Xavi Hernandez anamuhitaji. Kwa mujibu wa Bosi huyo, Xavi anahitaji kiungo mwenye umbo la kawaida mwenye ufundi zaidi kuliko matumizi ya mwili.

Pogba licha ya ufundi aliojaliwa, pia hutumia nguvu zaidi mchezoni, na Xavi anahitaji kitu tofauti hivyo staa huyu hakidhi vigezo vya Xavi Hernandez.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live