Kwa nini Enyimba anashiriki mashindano haya wakati ni wa (33) kwenye viwango vya (CAF).
Kwa nini timu namba 5, 6, 7,8 kwenye viwango vya (CAF) hazishiriki huku timu za 9,12 & 13 zikishiriki.
Hayo ni maswali niliyokutana nayo sana kutoka kwa wadau mbalimbali.
(CAF) walipanga msimu wa kwanza wa mashindano haya waanze na timu (24), kutokana na changamoto za ratiba na udhamini ikabidi wapunguze timu kutoka (24) hadi (8) kwa kuanzia msimu utakaofuata 24/25 wataalika timu zingine (16) ili ziwe (24).
(CAF) Walizingatia UKANDA katika kuzipata hizo timu (8) za kuanzia ndio maana baadhi ya timu bora zaidi ya baadhi ya timu zilizopo kwenye hizo (8) hazipo.
◉ North Africa — Al Ahly Cairo Wydad Casablanca, Esperance Tunis.
◉ South Africa — Mamelodi
◉ East Africa — Simba SC
◉ West Africa — Enyimba
◉ Central Africa — TP Mazembe
Awali ilichaguliwa klabu ya Horoya AC kuuwakilisha ukanda wa Africa Magharibi lakini hawakukidhi vigezo hasa kutokuwa na miundombinu bora (Viwanja) hivyo nafasi yao akapewa Enyimba.
01. 83 — Al Ahly Cairo
02. 74 — Wydad Casablanca
03. 56 — Esperance de Tunis
04. 51 — Mamelodi Sundowns
05. 51 — Raja Casablanca
06. 39 — Zamalek
07. 37 — RS Berkane
08. 36 — CR Belouzdad
09. 35 — Simba SC
10. 35 — Pyramids
11. 33.5 — Petro De Luanda
12. 31 — JS Kabylie
13. 30.5 — TP Mazembe
14. 29 — Horoya
15. 27 — USM Alger
16. 24 — Orlando Pirates
17. 23 — Al-Hilal Sudan
18. 20 — Young Africans
19. 20 — ASEC Mimosas
20. 19 — Etoile Du Sahel
21. 19 — ES Setif
22. 16 — Coton Sport
23. 15 — Marumo Gallants
25. 15 — AS Vita Club
26. 14 — CS Sfaxien
27. 13 — Al-Merrikh Sudan
28. 12 — Al-Ahly Tripoli
29. 12 — Al-Masry
30. 12 — FAR Rabat
31. 10 — Rivers United
32. 10 — US Monastir
33. 10 — Enyimba
34. 10 — MC Alger
35. 09 — Al Ittihad
36. 08 — Amazulu.
24/25 timu zitakazoshiriki zitakuwa (24) kwa kuzingatia vigezo hivi.
◉ Rank za CAF top 20+
◉ Klabu zenye mashabiki wengi.
◉ Klabu zenye miundombinu bora.