Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kwa mpira huu wa Gamondi, watu wataomba sana maji uwanjani

G Yanga Tizi Kwa mpira huu wa Gamondi, watu wataomba sana maji uwanjani

Fri, 25 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kwa mpira huu wa Yanga watu watapata kiu sana ya maji na wakikosa maji ya kunywa wataomba hata maji ya Kunawa hili wanywe maana wapo fiti sana Kuna muda wanafanya high pressing katika lango la mpinzani.

Mpira unatembea pasi nyingi soka la kasi kama haupo fiti ukitema mate yanaishia kifuani muda wote wanakimbia wanampiga presha mpinzani wao ukitaka kudhibitisha Hilo tazama mchezo wa Dabi katika fainali ya Ngao Yanga walichezea sana mpira kwa asilimia kubwa ni kwa sababu ya aina yao ya mpira wa sasa chini ya kocha wao Muargentina Angel Gamondi.

KMC wamekula goli Tano safi siyo kwa bahati mbaya wamezidiwa sana quality ya timu mbaka mchezaji mmoja mmoja kweli Wananchi wameanza ligi rasmi maana ndiyo mchezo wao wa kwanza walipata ushindi wa magoli mengi kuliko Timu yoyote wakiwa wamezidiwa mchezo.

KMC walizidiwa Kila idara huu siyo ushindi tu huu ni unyanyasaji huu ni ukatili umefanywa na Wananchi wa jangwani.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: