Huwenda ukawa ni moja kati ya watu walioshangazwa na maamuzi kutoka kwa mchezaji Lionel Messi baada ya kukataa ofa Kubwa ya dola Billion 1.9 ambayo ni zaidi ya Tsh trillion mbili za waarabu kutoka Saudia na kwenda kuchukua pesa kichele za wa-marekani kutoka Inter Miami ambayo inakadiriwa kuwa ni Dollar za ki-marekani Million 150 ambayo ni zaidi ya Billion 300.
Kama utakuwa ni sehemu ya washusha lawama na kuona kwamba Messi alifanya makosa kwenye machaguzi yake basi utakuwa unamkosea sana, Hizi hapa sababu za Messi kuchagua Inter Miami na sio Al-Hilal
Faida alizonazo ndani ya Inter Miami.
- Uwezekano wa yeye kununua timu.
- Kugawana mapato na APPLE TV wanaorusha matangazo ya michezo ya Ligi hiyo.
- Kugawana mapato na Kampuni ya Adidas ambao ni wavalishaji wa Timu.
- Na baadhi ya marupurupu mengine.
Kwa mgawanyo huo mapato anayoweza kuingiza ni zaidi ya ile Dollar Billion 1
Kilichobadilika kwenye Club ya Inter Miami tangu fununu za Messi.
- Gharama za mapato ya Ticket kuongezeka mara tano ya kawaida.
- Wanapata idadi ya Followers Laki Moja kwenye kila saa, kwenye instagram page yao ambayo kabla ya ujio ilikuwa na idadi ya wafuasi Million 1 kwa sasa inawafuasi Million 7.8
Mwisho japo sio kwa umuhimu kuna sababu za chini chini zinasema kwamba mke wa Messi hakupendezwa na kwenda kuishi uarabuni kutokana na tamaduni na maisha kuwa mageni kwake, ukilinganisha na marekani ambapo pia wanazungumza kihispania.