Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kwa mipango hii ya Yanga, mtapigwa sana tanotano

Yanga X640.png Kwa mipango hii ya Yanga, mtapigwa sana tanotano

Mon, 4 Sep 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

KWA sasa wale Yanga wamekuwa wa moto sana si mnaona matokeo ambayo wanayapata katika mechi zao yaani ni mazuri na soka lao linavutia.

Baada ya kuwaona kwenye Ngao ya Jamii kule Tanga pamoja na mechi ila ya siku ya kilele cha Wiki ya Mwananchi dhidi ya Kaizer Chiefs, tukaambizana kwamba huenda ni nguvu ya soda emu tusubiri basi msimu ukianza.

Sasa baada ya msimu kuanza ndio tunaona jamaa wamekuwa balaa zaidi hata ya walivyokuwa katika mechi zile za kupasha.

Jamaa wanacheza kitimu sana, wanashambulia kwa pamoja na wanazuia kitimu na ndio maana sio jambo la ajabu unaona wanafunga idadi kubwa ya mabao na hawaruhusu nyavu zao kutikiswa kirahisi.

Mechi tatu zilizopita wamepachika mabao 15, wakifunga mabao matano kwenye kila mchezo dhidi ya KMC, ASAS na JKT Tanzania.

Kinachoonekana timu nyingi hazina nidhamu ya mbinu zinapocheza na Yanga na ndio maana zinaonekana zinapigwa nyingi na pia hazifanyi tathmini ya kutosha ya ubora wa vijana hao wa Miguel Gamondi.

Kama timu yako ina wachezaji wa daraja la kawaida, haupaswi kupishana na Yanga, jitahidi kuziba mianya ya wao kupeleka mipira karibu na lango lako lakini unatakiwa kuhakikisha wachezaji wako wanakuwa fiti na wenye pumzi ya kutosha kwa dakika zote sa mchezo.

Ila kiukweli Yanga hii ya Gamondi sio ya kuichukulia poa kwa sababu kuna siku mtu ataingia aibuĀ  pale.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: