Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kwa mamilioni haya ya Al Ahly, Aziz Ki atabaki Yanga kweli?

Aziz Ki Al Ahly Yanga.jpeg Kwa mamilioni waliomwaga Al Ahly kwa Aziz Ki sidhani kama atabaki Yanga

Tue, 21 May 2024 Chanzo: Farhan Kihamu

Stephen Aziz Ki ana offer mbili kutoka Al Ahly na Orlando Pirates, amewapa Yanga unafuu wa offer ili aweze kusaini kwao na mahitaji yake kutoka kwa vyanzo vyangu anahitaji kiasi cha dola 500,000 ili aweze kusaini ikiwa ni sawa na tsh bilioni 1.2 za Kitanzania.

Mpaka hivi sasa Wananchi hawana kiasi hicho na klabu kwa mujibu wa vyanzo vyangu imejipiga mpaka Dola 350,000 za Kimarekani wapo tayari kumpa ila Aziz ameshikilia zifike 500,000 ili asaini, jitihada zinaendelea ila kinachohitajika ni huo mzigo.

Stephen Aziz Ki kwa offer alizonazo mezani ni lazima tu ataondoka kama ambavyo wengine wote waliowahi kuja nchini kwetu wakapata offer nono wakasepa zao, kikombe cha Clatous Chama, Fiston Mayele, Luis Miquissone na sasa Aziz tutaendelea kukinywa klabu za Kariakoo, yani Tanzania itawapa majina sana Wachezaji na mwisho ile peak wataenda kufaidi wengine.

Kama hampendezwi na hali hii basi wa kubadilika sio Matajiri bali sisi wenyewe Walala Hoi, inaanza na mindset! Tupo tu hapo tunapiga kelele kuwa Aziz abaki na hatuna kadi, jezi za klabu hatuna na kama tunazo basi moja, hauna merchandise zingine, hulipii Uanachama na hata kadi ya Shabiki huna na uwanjani mbinde unataka kiingilio kidogo.

Leo mtashangilia kwakuwa tunabahatika kupata mbadala, ipo siku soko litatupa surprise na hizi timu zitajifia kifo cha asili huko Kimataifa, tutashikana uchawi hapa! Mindset Mindset Mindset! Mashabiki na Wanachama mpira ni biashara katiki ni UBEPARI hawa wenzetu wa Kimataifa inapokuja offer hawawazi mara mbili, ukitaka abaki weka offer kama hiyo.

Mpaka hivi sasa Aziz hajasaini karatasi yoyote ndani ya Jangwani.

Chanzo: Farhan Kihamu