Tanzania (Taifa Stars) inahitaji alama moja tu mbele ya Algeria ikiwa ugenini ili ifuzu Afcon 2024, Kocha mkuu wa kikosi cha Stars Amarouche ameita nyota wake watakaofanya hiyo kazi.
Kwa aina ya mashabiki zetu walivyo ikitokea hajafanikiwa kufuzu basi lawama zote zitakuwa juu yake na sababu kubwa zikiwa ni kuwaacha baadhi ya nyota wao akiwemo Kapombe na Zimbwe Jr.
Binafsi naamini katika maamuzi ya kocha na naamini wataenda kupata matokea mazuri huko Algeria, na nyota walioitwa naamini watapambana kuandika historia nyingine kwa Taifa lao.
Hata ikitokea hatujafuzu naomba isiwe sababu ya kocha kusemwa au kufukuzwa bali iwe sababu ya kumpa muda atengeneze kile anachokitaka kwa manufaa ya Taifa na soka letu.