Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kwa jambo hili, Yanga inazingua

Eng. Hersi Sdv Rais wa Yanga, Injinia Hersi Said

Thu, 22 Aug 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Yapo mambo ambayo Yanga haipaswi kuyafanya hivi sasa kutokana na daraja ambalo ipo katika soka hapa nchini na Afrika kijumla.

Miongoni mwa hayo ni hili la kuacha wachezaji kiholela na kuchelewa kulipa klabu zinazoiuzia wachezaji katika dirisha la usajili na kusababisha kushtakiwa katika Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa).

Inapaswa kuyaepuka kwa vile sasa hivi imeshafikia daraja la kuwa miongoni mwa timu kubwa barani Afrika na hili wala halihitaji ubishani maana ni mwaka jana tu ilitinga fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika.

Ukubwa huo unapaswa kuthibitishwa kwa vitendo kwa kufanya mambo kiweledi na katika utaratibu sahihi na sio kukurupuka kama ambavyo imefanya katika usajili na kuachana na baadhi ya wachezaji ambao ndio wameiingiza katika kesi hizo.

Kukurupuka kunaweza kutafsiriwa kwa sababu sajili zilizoiingiza Yanga matatani ukizitathmini kwa kina nyingi utabaini hazikuwa na ulazima kwa vile tayari kulikuwa na wachezaji kwenye nafasi hizo ambao walifiti vyema na walioletwa ingekuwa ngumu kupata nafasi mbele yao.

Mfano miongoni mwa wachezaji walioitia Yanga matatani ni winga kutoka Ghana, Augustine Okrah ambaye alisajiliwa na Yanga dirisha dogo la usajili akitokea Bechem ya huko kwao.

Wakati Yanga inamsajili Okrah, tayari kikosini ilikuwa na Stephane Aziz Ki na Maxi Nzengeli ambao walikuwa ndio tegemeo la timu na chaguo la benchi la ufundi katika idadi kubwa ya mechi za timu hiyo.

Hata hivyo, kabla ya kujiunga Yanga, Okrah aliwahi kucheza hapa nchini katika timu ya Simba na hakuondoka vizuri baada ya kuachwa kwa sababu za utovu wa nidhamu ambao ulikithiri.

Hilo lilipaswa kuifanya Yanga kujiongeza na kutohangaika na mchezaji huyo lakini cha kushangaza ikalazimisha usajili wake na yakaja kutokea ya kutokea hadi kusababisha leo hii kushtakiwa na mchezaji pamoja na klabu yake iliyowauzia.

Chanzo: Mwanaspoti
Related Articles: