Yanga walianza kumuuguza mchezaji wao Yacouba Songne ambaye alikuwa na majeraha kwa muda mrefu hadi akapona, akacheza mashindano ya Mapinduzi Cup lakini inaonekana benchi la ufundi lilimshauri atafute timu nyingine kutokana na ushindani wa nafasi uliopo kwa sasa kikosini.
Yacouba akajiunga na Ihefu na sasa anafanya vizuri ikiwa ni pamoja na kuchaguliwa mchezaji bora wa mwezi Februari baada ya kufunga magoli mawili na kutoa assist moja katika mechi mbili alizocheza mwezi huo.
Sasa hivi tunaona Hassan Dilunga amerejea kwenye kikosi cha Simba baada ya kuwa nje kwa muda mrefu akiuguza majeraha ya goti.
Kwa hiyo benchi la ufundi baada ya kuona uwezo wake litatoa mapendekezo yake ya kiufundi ili Dilunga aendelee kubaki Msimbazi au aruhusiwe kwenda mahali pengine.
Ni ustaarabu na utaratibu mzuri klabu kitu ambacho Azam FC wamekuwa wakikifanya kwa muda mrefu sana.