Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kwa hili la Fei Toto! Yanga wakae mkao wa kula

Fei Toto Feisal Salum

Sat, 18 Feb 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Anarudi. Yanga imebakiza hatua chache kumaliza vita yao kikubwa dhidi ya kiungo, Feisal Salum 'Fei Toto' baada ya jana kumrudisha jijini Dar es Salaam kwa mazungumzo ya mwisho ya kumrudisha kundini na baada ya hapo suala la Jumapili ataachiwa kocha Nasreddine Nabi.

Iko hivi. Bosi mmoja wa juu wa Yanga ndiye aliyesimamia mazungumzo hayo na baada ya vikao vya kisiwani Zanzibar jana kiungo huyo alitakiwa kuvuka maji kwa safari maalum ya kuja kuonana na tajiri wa Yanga Ghalib Said Mohamed na Rais wa Yanga, Injinia Hersi Said ambaye amerejea jana nchini kutoka Makka, Saudi Arabia akikoenda kwa ibada ya Hija.

Mezani kwa Yanga ukiachana na suala la kumaliza tofauti za pande hizo mbili lakini jingine ni kuangalia uwezekano wa kumpa mkataba ambao unaonekana kuwa wa kufuru kiungo huyo.

Kama Feisal atakubali dili hilo anaweza kuwa staa wa Kitanzania tajiri zaidi baada ya Yanga kufikiria kumpa mshahara wa sh 16.5 milioni kwa mwezi, huku dau lake la usajili ukijumlisha na gari linaweza kukaribia sh 400 milioni.

Hata hivyo, jana Mwanaspoti lilimtafuta Fei Toto, lakini alishindwa kukubali au kukataa huku akiishia kucheka na kuomba kwanza afike jijini Dar es Salaam. Yanga kupitia Makamu wake wa Rais Arafat Haji ameliambia Mwanaspoti kuwa haitakuwa kitu kipya kumuona Fei Toto uwanjani Jumapili kwa kuwa huyo ni kiungo wao na mali yao.

Arafat aliongeza na kukiri kuwa walikuwa katika mazungumzo ya kina na familia na hata mchezaji mwenyewe juu ya mustakabali kwake huku akisema Yanga hii haiwezi kushindwa kitu.

"Ukiniuliza kuhusu Feisal jibu langu litakuwa moja tu huyu ni mchezaji wetu, na kuhusu kucheza au kuwepo Jumapili ni suala la uamuzi wetu na makocha kwa kuwa huyu ni mwanafamilia na sherehe yetu ya Jumapili inamuhusu,"alisema Arafat. Nabi ampa ratiba ya tizi

Mmoja wa wanafamilia wa Fei Toto amelipa uhakika Mwanaspoti, huku akionyesha kwa ushahidi makaratasi ambayo kiungo huyo alikuwa anapewa mazoezi muda mrefu na makocha wa Yanga chini ya Nasreddine Nabi.

Mwanaspoti wiki iliyopita lilifichua juu ya Fei Toto kupigiwa simu na kocha Nabi na kuzungumza kwa dakika 43, jambo kocha huyo alikiri, lakini kiumbe moja ya mazungumzo hato yalikuwa ni kumpa ratriba ya tizi na kiungo huyo amekuwa akiifanya kimyakimya.

Mmoja wa kaka wa mchezaji huyo aliyesema, Nabi alikuwa kila wakati anaongea na Fei Toto akimhoji na kutaka ushahidi wa video jinsi alivyokuwa akitekeleza programu hizo.

"Fei alikuwa anafanya mazoezi makali sana hakuwa ana anaamka anakula na kulala, nakuonyesha haya angalia hizi ni programua ambazo zote zilikuwa zinatoka Yanga hapo hapo, huu ni ushahidi kwamba huyu kocha alikuwa anamuheshimu sana ndugu yetu," alisema kaka huyo.

Chanzo: Mwanaspoti