Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kwa heri wanetu!

Faridi Muda Kwa heri wanetu!

Wed, 13 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Juzi tu hapa Nkane, Mdathir, Sureboy, Farid Mussa, Moloko, Kibwana, Walikuwa ni wachezaji hatari sana hata kama walikuwa wanatokea Sub, ukianza kuhesabu magoal ya ushindi au perfomnce zao bora hapa hutoacha kukumbuka.

Nkane aliipatia Yanga goli la kuwapa taji la ASFC 2021/22, baada ya ku-level Score board 3-3 kisha mikwaju ya penalti ikaamua, bado Nkane aliendelea kupata nafasi kwenye Kikosi cha Nabi na alikuwa anafanya vyema sana.

Mdathir, aliwapatia Yanga goal la kuongoza dhidi ya TP Mazembe CAFCC, na lile goli lilichukua goli bora la group stage CAFCC, bado alikuwa na kiwango bora sana majuzi juzi.

Sureboy, Master, Atakumbwa kwa kiwango kizuri alichokionesha kwenye mchezo wa kufuzu Group stage dhidi ya Club African, ugenini lakini mwamba ile match aliwaka sana na bado alikuwa ni mchezaji mzuri sana

Farid Musa 'Baller Dancer' anayecheza namba nyingi pale Yanga, Beki wa kushoto , Winger wa kushoto, Middle aliwahi kuwapatia points 3 mhimu Yanga dhidi ya TP Mazembe ugenini

Moloko, moja ya winger nzuri kabisa na hatari sana, aliwahi kuwafungia goal la pili Yanga kwenye mchezo dhidi ya Real Bamako kwa mkapa.

Kibwana Shomary, si kulia si kushoto kote kote mdogo wangu anakaba na anashambulia ni kweli kazini kwake kuna kazi ila naye ni mzuri matches dhidi ya Dodoma Jiji, matches dhidi ya Al Merrikh ushashinda tayari na umefuzu naye anastahili kucheza

Ukiifuatilia Yanga, ilikuwa ni timu ambayo kila mchezaji alikuwa ni hatari kulingana na Sub aliyokuwa anafanyiwa, lakini Yanga ya sasa hawapati nafasi kinachoendelea ni nini?

Timu ya Taifa itarudi kule kule tulipotoka hakuna wachezaji wapya watakaoitwa maana kibwana sasa hawezi kuitwa maana sub kila mechi. Yanga ya msimu huu inaweza kuwa ndiyo Yanga nzuri kuishuhudia.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live