Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kwa heri Basena, tuliyajua mapema

Basena Ihefu.png Mganda Moses Basena

Fri, 8 Dec 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Ni wachache sana wanaoweza kushangaa uamuzi wa Ihefu kumfukuza kocha Moses Basena kutoka Uganda ambaye amehudumu katika muda usiofika hata miezi miwili.

Ilikuwa iko wazi kwamba Basena asingeweza kudumu kwa muda mrefu pale Ihefu kutokana na hulka na misimamo yake pamoja na zile za wachezaji wa Kitanzania.

Basena ni kocha mkali ambaye huwa hapendi wachezaji magoigoi na wasiotambua wajibu wao katika timu iwe wakati wa mechi au muda wa mazoezi naye mara zote amekuwa akitaka wachezaji kuvuja jasho na kucheza kwa kujitolea kwa ajili ya timu.

Sio kocha ambaye anaweza kuwalea wachezaji wasio siriaz na huwa hayuko tayari kuona kuna mchezaji anakuwa zaidi yake kwenye timu na ikitokea hivyo kuna mawili, aondoke yeye au mhusika aondoke.

Sasa wakati Basena akiwa na hulka hiyo, wachezaji wetu wengi wa sasa wanapenda kulelewa kama mayai na wana tabia ya kutaka kunyenyekewa na mashabiki, viongozi au makocha hata kama hawana kiwango bora uwanjani.

Ikitokea wana kocha mkali na ambaye anasimamia misingi ya kinidhamu kwenye timu na pia awe mtu wa mazoezi, kinachofuata hapo ni kuanza kwa mipango ya kumkwamisha ili aje yule ambaye wao wanaamini watammudu na kumfanya atakavyo na usiombe hao wachezaji wawe na urafiki na viongozi.

Kwa vile wanajua ni ngumu wao kufukuzwa, watacheza chini ya kiwango na kuifanya timu isipate matokeo mazuri kwani hiyo itakuwa sababu tosha ya kushawishi uongozi umtimue mwalimu na hilo tumeliona katika timu nyingi na kwa muda mrefu.

Naamini jamaa walichangia kumpigisha shoti Basena kwa uongozi kama ilivyotangulia kwa makocha wengine wawili ambao waliiongoza timu kabla yake.

Haiwezekani makocha watatu tofauti wakawa hawana jipya kwenye timu kabla hata msinmu haujafika nusu, kuna jambo linaloendelea kwa wachezaji pale lishughulikiwe.

Chanzo: Mwanaspoti