Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kwa bilioni 2 za kujenga Uwanja amekurupuka, MO atakiwa kusoma alama za nyakati

Mo Simba Dewji Mohammed Dewji "Mo Dewji"

Tue, 14 Dec 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Japokuwa wapenzi na Mashabiki wa Simba wanaweza wasikubali na wakaungana nae kwa asilimia 100.

Lakini kuna nyakati inabidi ukubali ukweli hata kama unakuumiza, kwa kuwa ukweli ni ukweli kwa lugha yoyote ile.

Dunia inabadilika, maendeleo ya teknolojia yanakua, hiyo pia imechangia hata tabia za watu kubadilika.

Kila kizazi kina tabia na life style yake, ndiyo maana huwa ni kawaida kusikia wale ambao wamepitwa na kizazi husika utawasikia wakitamka: “Enzi zetu sisi…”

Ukitaka kufurahia maisha changanya hiyo ‘enzi zenu’ na enzi za sasa kisha tumia akili yako kuchuja, utaishi vizuri.

Mohammed Dewji ‘Mo’ amefanya makubwa mengi kama wenzake enzi za kina Azim Dewji, Abbas Gulamali, Yusuf Manji na wengine wengi.

Kutompa sifa zake kwa makubwa mengi aliyoyafanya hasa kwa Simba, itakuwa ni kumkosea heshima.

Jambo moja kubwa ni kuwa Mo Dewji anatakiwa kusoma alama za nyakati, mambo yamebadilika zile zama za kuambiana porojo za soka, kwa sasa zime ‘upgrade’, kuna njia mpya za kupata ‘publicity’ na ‘sympathy’ (kujitangaza na kupata huruma ya jamii).

Teknolojia imekifanya kizazi cha sasa kuwa cha kisasa zaidi, hivyo vyovyote ambavyo yeye ama mtu yeyote anapofanya porojo katika masuala ya ‘serious’, ni rahisi kushambuliwa na hata kuumbuliwa.

Kwa hadhi yake nafikiri imefika hatua hatakiwi kuwa mtu wa kuzungumza sana hadharani hasa katika mambo ambayo anajua ama ni magumu kutekelezeka au anaweza kutoaminika.

Mo amefanya mengi makubwa, hana haja ya kutumia nguvu kubwa yeye binafsi kuonyesha, afanye vitendo kisha ‘wapambe’ wapige domo kwa kile anachokifanya.

Kauli ya kusema kuwa yupo tayari kutoa Sh bilioni 2 za kujenga uwanja ikiwa ni muda mfupi baada ya tukio la kiongozi wa Simba kuzuiwa uwanjani, ni wazi inaonyesha ni kauli za mihemko.

Mo aliwahi kutangaza kujiondoa Simba SC kwa post ya mtandaoni, alikomenti katika ukurasa wa Clatous Chama vitu vya ajabu.

Kauli za mashabiki mitandaoni akiwemo yule aliyekuwa mtumishi wao klabuni ni kama zinamjaza upepo na kumtoa mstarini. Kwa hadhi yake hatakiwi kuwa levo hizo za mihemko.

Kwa faida ya heshima yake, ni vema akaamua kukaa kimya kisha vitendo viongee, washauri wake wasiogope kumwambia kuwa ‘mzee unachemka’.

Awape kazi hiyo ‘chawa’ watamsafisha na kumpromoti zaidi ya anavyofanya sasa, tofauti na hapo sioni kesho yake nzuri kwa ‘public’.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live