Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kwa Yanga hii, msala umebaki kwa Gamondi tu

Gamondi Kambi Kwa Yanga hii, msala umebaki kwa Gamondi tu

Tue, 25 Jul 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Mashabiki wa Yanga kwa sasa wanasubiri kuona ni nini Kocha Gamondi ambaye tayari ameshaanza kazi, atafanya na ufundi wake na kutengeneza kikosi imara kitakachoendeleza moto msimu ujao.

Gamondi ana kazi ya kuendeleza moto wa Yanga hasa kutokana na upinzani utakaoonyeshwa na Simba na Azam FC ambazo kwa sasa zimejichimbia kwenye kambi zao zikijiandaa na msimu mpya.

Anatakiwa kuongeza makali zaidi ya aliyofanya mtangulizi wake, Nasreddine Nabi ili kuifikisha Yanga mbali zaidi na hasa kwenye michuano ya Afrika na itashiriki Ligi ya Mabingwa Afrika na msimu uliopiota ilicheza fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika.

Pia ana kazi ya kuhakikisha anatetea mataji ya timu hiyo iliyoyabeba kwa misimu miwili ikiwa chini ya Nabi kuanzia Ngao ya Jamii, Ligi Kuu Bara na Kombe la Azam Sports Federetion Cup (ASFC).

Kwa sasa kocha huyo na jeshi lake wanarudi kambini na kazi kubwa ni kuhakikisha inarekebisha makosa yaliyoonekana kwenye mchezo huo wa kirafiki juzi Kwa Mkapa ili kuanza msimu mpya kwa kishindo na kuonyesha kwa 'Amakhosi' haikuwa bahati mbaya.

Chanzo: Mwanaspoti
Related Articles: