Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kwa Ubingwa, Bado sana

Mn City Man City wakishangilia moja ya magoli yao usiku wa jana

Sun, 1 May 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Manchester City imerudi tena kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu England baada ya kuifunga bao 4-0 Leeds United katika mchezo uliochezwa Leo Jumamosi dimba la Elland Road.

Kabla ya mechi ya Man City, Liverpool walikuwa wamekwea kileleni kufuatia kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Newcastle United mchezo wa mapema Leo, hata hivyo City wametoa majibu sahihi katika mbio za ubingwa wa EPL.

Mabao ya City yamefungwa na Rodri akimalizia mpira wa kutengwa wa mshambuliaji wa kimataifa wa England Phil Foden kisha mchezo ukaenda mapumziko kwa bao moja.

Kipindi cha pili, mlinzi wa zamani wa Bournemouth Nathan Ake akafunga bao la pili akimalizia mpira uliopotea wa beki Ruben Dias.

Foden alisaidia tena kupatikana kwa bao la tatu ambalo limefungwa na mshambuliaji wa Kibrazil Gabriel Jesus kisha kiungo mkabaji Fernadinho akafunga bao la nne na kufanya matokeo kuwa 4-0.

Tofauti ya pointi baina ya City na Liverpool ni alama moja ambapo mechi nne zimesalia kabla ya kutamatika kwa kandanda nchini England.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live