Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kwa Tusker! Uje umejipanga

Tusker Pic Kwa Tusker! Uje umejipanga

Thu, 15 Dec 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Unaambiwa usije kichwa kichwa unapoikabili Tusker FC kutokana na dozi baada ya dozi wanazotoa katika Ligi Kuu Kenya iliyoingia raundi ya nne mwishoni mwa wiki iliyopita.

Kulikuwa na hatihati ya mechi za ligi kuchezwa kufuatia uamuzi uliyotolewa na Mahakama ya Utatuzi Migogoro Michezoni (SDT) ikipinga uamuzi wa Kamati ya Utendaji Shirikisho la Soka Kenya (NEC-FKF) kufutilia mbali msimu uliyopita hivyo kuinyima fursa APS Bomet na Fortune Sacco kucheza FKFPL baada ya kupanda kutoka Supaligi ya Taifa.

Hata hivyo ngarambe za FKFPL ziliendelea na mabingwa watetezi Tusker FC wanafanya biashara asubuhi wakijuafika jioni ni muda wa hesabu baada ya Jumamosi iliyopita kushinda mechi yao ya nne mfululizo wakiwa wameshuka dimbani mara nne hivyo kutoa onyo kwa timu yoyote inayodhamiria kuchukua ubingwa wa msimu huu.

Bao pekee la Tusker FC wakicheza ugenini katika Uwanja wa Thika dhidi ya Bidco United, lilifungwa na beki Clyde Senaji licha ya mabingwa hao kuwakosa wachezaji wanne muhimu akiwemo nahodha Humphrey Mieno ambaye yuko darasani akichukua kozi ya ukocha.

“Ninafuraha tumefanikiwa kupata pointi tatu muhimu, wachezaji wamekuwa wakijituma mazoezini na kukionyesha uwanjani wakati wa mechi,” alinukuliwa kocha wa Tusker FC, Robert ‘Simba’ Matano.

Ilikua ni mechi ya pili mfululizo kipa Patrick Matasi ambaye ametuliza boli baada ya sekeseke lake kutaka kuondoka akihusishwa na Kenya Police FC anaweka ‘clean sheet’.

Kipigo hicho ambacho ni cha pili mfululizo licha ya kuanza msimu kwa ushindi, hakikumfurahisha kocha wa Bidco United, Anthony Akhulia, ambaye alisema wanapoteza mechi kirahisi.

Akhulia alitarajia vijana wake wangezinduka baada ya kichapo cha mabao 2-1 kutoka kwa Gor Mahia lakini walipoteza nafasi za wazi dakika za mwisho.

Nako katika Uwanja wa Bukhungu kaunti ya Kakamega, ‘home coming’ ya Bernard Mwalala iliishia na kuondoka na pointi moja dhidi ya mabosi wake wa zamani, Kakamega Homeboyz, ambao walitangulia kupata bao lililofungwa na Michael Isabwa kabla Hillary Simiyu kuisawazishia Ulinzi Stars.

Bao hilo la Simiyu linamfanya kufikisha mabao matatu msimu huu sawa na Deogratious Ojok wa Tusker FC hivyo kuanza mapema kunogesha mbio za Kiatu cha Dhahabu.

Katika mbio hizo yumo pia Boniface Munyendo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live