Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kwa Simba hii, wataomba poo

Morisson Full Pictuer Wafungaji wa Mabao ya Simba dhidi ya Red Arrows

Sun, 28 Nov 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Hakuna sifa ambayo unaweza kuacha kuwapa Wekundu wa Msimbazi siku ya leo baada ya kuigaragaza vibaya Red Arrows ya Zambia katika mchezo wa Kombe la Shirikisho Barani Afrika na kuibuka na ushindi wa magoli 3-0.

Simba watakua na kazi ngumu ya kuhakikisha wanafuzu hatua ya makundi kwa kuhakikisha wanalinda ushindi wao wa leo watakaposafiri kuwafuata Red Arrows nchini Zambia katika mchezo utakaopigwa Disemba 5.

Katika mchezo huo wa leo magoli ya Simba yamefungwa na Bernard Morisson aliefunga magoli mawili na meddie Kagere.

Morisson amehusika katika magoli yote ya mchezo wa leo akifunga mawili na kutoa pasi ya goli kwa Meddie Kagere, lakini pia alikosa mkwaju wa penati katika mechi ya leo.

Simba walitawala asilimia kubwa ya mchezo wa leo, na walitengeneza nafasi nyingi za magoli ambazo walishindwa kuzitumia na kuzibadilisha kuwa magoli.

Hali ya Uwanja haikutpoa nafasi ya kuchezwa mpira wa burudani kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha Jijini Dar.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live