Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kwa Simba hii, jiandaeni vizuri kisaikolojia

Simba SC Saikolojia Kikosi cha Simba SC

Thu, 23 Feb 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kwa mujibu wa mtandao maarufu wa kutunza takwimu wa 'football database', Simba ni klabu ya 14 kwa ubora Afrika nyuma ya Horoya na Petro de Luanda ya Angola.

Kwa gepu dogo lililopo kati yao huwezi kutegemea mechi rahisi wanapokutana Simba na Horoya. Simba alipoteza ugenini dhidi ya Horoya, kipi kigeni hapo kwa soka la Afrika? As Vita wao walipoteza nyumbani dhidi ya de Luanda!

Raja Casablanca ni klabu ya nne kwa ubora Afrika wakiwa na pointi 1584! Ni gepu la takribani pointi mia kati yao na Simba. Umetafiti thamani na malengo ya Raja msimu huu?

Wao lengo lao ni kutwaa ubingwa wa Afrika kwa ngazi ya vilabu na taji ya ligi kuu Morocco. Kikosi chao kina thaamani mara ya 10 zaidi ya kikosi cha Simba. Unategemea mechi ya aina gani ukicheza dhidi yao?

Raja anaweza kusafiri kwenda Misri au Afrika Kusini na kushinda dhidi ya mkubwa kama Zamalek au Mamelodi Sundowns, na bado haitakuwa story. Kwanini kushinda dhidi ya Simba iwe story?

Azam?? Azam yupo tatu bora ya vilabu nchini. Wana kikosi imara kilichojaza wageni wenye vipaji vikubwa kama ilivyo Simba. Mechi kati ya Azam na Simba, huwezi kulala ukitegemea mechi rahisi.

Simba wamecheza mechi tatu ngumu dhidi ya wapinzani imara. Hata sasa hivi wakiwa safarini Uganda wanakwenda kucheza mechi nyingine ngumu ambayo haitashtua kama hawatapata matokeo. Ni uhalisia wa mpira ulivyo!

Yote tisa, kumi wapo na kocha mgeni! Anahitaji muda kufundisha na kueleweka, labda msimu ujao ndipo unaweza kumdai mafanikio. Unakumbuka Nabi alianza vipi Yanga??

Unaniambia mbona Sven na Gomes walikuja na hawakuhitaji muda? Jibu ni rahisi, tazama kikosi alichorithi Robertinho na kikosi walichorithi akina Sven.

Simba hii ina Miquissone? Sifikiri kama Simba hii ina Meddie Kagere. Sidhani kama John Bocco huyu ni yule wa misimu mitatu nyuma. Sioni kama Inonga na Onyango wana ubora ule wa Erasto na Sergie Wawa.

Lakini ebu tazama katika ligi wapinzani wa Simba walivoimarika. Yanga imeenda juu kiasi gani kutoka kwa Ditram Nchimbi hadi kwa Fiston Mayele? Kocha wa Yanga amekaa muda gani?

Nadhani mashabiki wa Simba wanaomlalamikia kocha hawafahamu mafanikio katika soka sio mchakato wa usiku mmoja.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live