Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kwa Nabi! Gamondi master

NABI GAMONDI MS Kwa Nabi! Gamondi master

Fri, 16 Feb 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Wakati kikosi cha Yanga kikitua Mkoani Morogoro kikiwafuata KMC kuanza mzunguko wa pili wa Ligi Kuu Bara kocha wao Miguel Gamondi rekodi zinambeb a dhidi ya mtangulizi wake Nasreddine Nabi.

Ukiangalia takwimu za mzunguko wa kwanza tu zile za Nabi wakati akiwa Yanga na hizi za sasa timu hiyo ikiwa chini ya Gamondi, Muargentina huyo amempiku mtangulizi wake.

Msimu wa 2022/23 ambao Nabi ulikuwa wa mwisho kwake akiwa na Yanga akimaliza ligi kwa mafanikio, kocha huyo kwenye mechi 15 alishinda mechi 12 wakati Gamondi akishinda 13 akimzidi kwa mchezo mmoja.

Gamondi kwenye mechi hizo 15 alipomuacha Nabi ni baada ya kutoa sare moja pekee dhidi ya Kagera Sugar ugenini kwa kutofungana, wakati Nabi akitibuliwa na Simba na Mbeya City alipolazimishwa suluhu nyumbani kila mchezo huku makocha hao wakajikuta wanatibuliwa na timu moja Ihefu wote wakipoteza dhidi ya timu hiyo kwa mabao 2-1 ugenini.

Gamondi akamaliza mechi 15 akiikusanyia Yanga pointi 40 zilizotokana na kushinda mechi 13 zikimpa jumla ya alama 39 huku alama moja akiiongeza kupitia sare ya Kagera na kufanya jumla ya alama 40 huku Nabi alimaliza mechi zake hizo na jumla ya alama 38.

Yanga ya Gamondi ilianza ligi kwa kishindo ikiwa inatoa vipigo vikali ambapo kwenye mechi zake mbili za kwanza ilitengeneza mabao 10 na ndani ya mechi 15 ikatengeneza mabao 36 ya kufunga wakati Nabi nusu ya msimu huo alitengeneza mabao 27 Mtunisia huyo akizidiwa mabao 9 lakini makocha wote wakagongana tena kwa timu zao kuruhusu mabao 8 kila mmoja.

Mabao hayo ya kufunga na kufungwa yakambeba tena Gamondi kwa utofauti ambapo akawa na tofauti ya mabao 28 akimzidi Nabi ambaye alibaki na tofauti ya mabao 19 huku pia kwa mara ya tatu makocha wote wakagongana kwa kuwa na mechi 9 kila mmoja ambazo hawakuruhusu mabao.

Kiungo mshambuliaji wa zamani wa Yanga, Sekilojo Chambua akizungumzia utofauti huo wa makocha hao wawili alisema kitu kikubwa ambacho kimembeba Gamondi ni kuwa na watu tofauti wanaojua kufunga tofauti na Nabi ambaye kikosi chake kilikuwa kinamtegemea aliyekuwa kinara wa ushambuliaji Fiston Mayele pekee.

“Nadhani Gamondi alikuja na utofauti juu ya kikosi chake, alitengeneza timu ambayo yoyote anaweza kufunga, kikosi hiki cha msimu huu watu tiofauti wamekuwa wanaweza kuitengenezea ushindi timu, wapo washambuliaji wamekuwa wakifunga, viungo na hata mabeki,”alisema Chambua.

“Hili lilikuwa tofauti na wakati wa Nabi tulikuwa tunaona timu inamtegemea mfungaji mmoja pekee Mayele kwenye kufunga, wengine walikuwa wanafunga lakini kwa uchache sana nadhani hilo ndio lilikuwa kubwa.”

Naye winga wa zamani wa Yanga, Said Maulid SMG ambaye pia ni kocha alisema; “Kitu cha kwanza kikubwa kiufundi Gamondi amefanikiwa timu yake kufunga zaidi kutokana na watu kuwa na ubora wa kufunga, Nabi timu yake ilikuwa inategemea hasa nguvu ya Mayele shida inakuja kwamba siku huyo mtu mmoja akikutana na ugumu mambo yanakuwa tofauti.”

“Kitu kingine muhimu ni kwamba makocha wote hawa walikuwa wanatumia mfumo mmoja lakini utekelezaji wake uwanjani ndipo walipokuwa wanatofautiana,Nabi timu yake ilikuwa taratibu kidogo inapotengeneza mashambulizi lakini Gamondi timu yake inaposhambulia imekuwa na kasi zaidi.

“Angalia pia inapoutafuta mpira kazi ya kuupokonya imekuwa ikifanyika kwa haraka sana hii imekuwa inazipa ugumu timu pinzani kwani zinakuwa bado hazijajipanga sawasawa.”

Chanzo: Mwanaspoti
Related Articles: