Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kwa Mkapa ulinzi wa viwango

Mkapa Ulinziiii Kwa Mkapa ulinzi wa viwango

Fri, 20 Oct 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Mpaka sasa ulinzi na usalama ndani na nje ya uwanja wa Benjamin Mkapa umeimarishwa kwa kiwango kikubwa.

Licha ya mashabiki kuzidi kuongezeka na askari pia wanaendelea kuhakikisha hakuna vurugu yoyote wakati wakiendelea kuingia uwanjani.

Askari waliotawala kila maeneo wengine wanaonekana kuwa na farasi, virungu na silaha za moto yote hayo ni kuhakikisha usalama unaimarika

Mistari mirefu ya foleni za mashabiki inaonekana uwanjani hapa huku kukiwa hakuna changamoto yoyote iliyojitokeza mpaka sasa.

Wakati mashabiki wakiwa kwenye mistari Polisi nao wamekuwa wakifanya kazi yao kwa viwango kwa kuzuia kila anayeingia uwanjani hana kitu chochote kinachoweza kuvunja amani.

Upekuzi mkubwa umekuwa ukifanyika na kama uko njiani inakuja Uwanja wa Benjamin Mkapa kushuhudia mechi kubwa kati ya Simba dhidi ya Al Ahly huku ukiwa umebeba maji yako au kinywaji chochote hakikisha kinaisha kama hujafika getini kwani utakiacha hapo.

Mashabiki wenyewe wameonekana kuwa na mzuka wakati wanaingia viwanjani huku rangi zinazotawala hapa ni zile zenye jezi za timu ya Simba ambazo ni nyekundu, nyeupe na buluu kwa uchache.

Chanzo: Mwanaspoti
Related Articles: