Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kwa Messi kuna mengi ya kujifunza

Messi Taye Obi (14).jpeg Kwa Messi kuna mengi ya kujifunza

Tue, 7 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Pichani ni wanafainali na wachezaji bora wa Mashindano ya Dunia ya Mpira wa Miguu upande wa vijana chini ya miaka 20 (FIFA World Youth Championship), yaliyofanyika katika ardhi ya Uholanzi, mwaka 2005.

Timu ya taifa ya Argentina walitwaa ubingwa huo mbele ya Nigeria, kwa mbao 2-1. Lionel Messi ‘Lapulga’ akawa ndio mchezaji bora wa mashindano hayo na kutwaa medali ya dhahabu, nyuma ya John Obi Mikel aliyetwaa medali ya silva na Taye Taiwo kutwaa medali ya shaba.

Miaka 18 mbele, Messi ametwaa tuzo ya mchezaji bora wa dunia ‘Ballon d’or’ mara nane.

Upande wa Mikel tayari ameshatundika daruga ilhali, Taye anasaka malisho ya jioni katika klabu ya Salon Palloilijat ya nchini Ufini ama Finland.

Unadhani ni kipi kinawakwamisha wachezaji wa kiafrika kudumu katika soka la ushindani kwa muda mrefu?

Chanzo: www.tanzaniaweb.live