Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kwa Medo ni suala la muda

Melis Medo Dodoma.jpeg Mellis Medo

Fri, 4 Nov 2022 Chanzo: Mwanaspoti

Kocha wa Dodoma Jiji, Mellis Medo amesema wakati anachukua mikoba ya kufundisha timu hiyo alikuwa kwenye wakati mgumu kutokana na kukosa muda wa kufanya mazoezi kwa utulivu wachezaji.

Akizungumza Medo alisema alipoichukua timu ndani ya siku sita aliiongoza katika mechi mbili ngumu dhidi ya Ihefu ugenini na Mtibwa Sugar nyumbani ambazo zote alipoteza.

Alisema bahati nzuri kwake wakati huu amepata siku sita za kufanya mazoezi mengi ya mbinu pamoja na kurudisha morali ya wachezaji iliyoonekana kuwa chini baada ya kushindwa kufanya vizuri kwenye Ligi Kuu Bara.

“Nimewaambia kila mchezaji anapaswa kuweka akilini kupambana kwa ajili ya timu ili kushinda michezo iliyo mbele yetu. Suala la kucheza kwa morali ya chini halitakiwi kuwepo tena,” alisema Medo aliyewahi kuzifundisha Coastal Union na Gwambina.

“Kwenye mazoezi ya siku hizo sita kwa kiasi kikubwa wachezaji wameonyesha mabadiliko na kupokea mbinu. Maelekezo niliyowapatia naamini tunakwenda kubadili huu upepo mbaya na kuanza kupata matokeo bora.

“Kikosi kina wachezaji wazuri na wenye vipaji ila morali ilikuwa chini huku wengine hadi kushindwa kucheza kutokana na maelekezo waliyopatiwa na benchi la ufundi, nadhani kwa sasa hilo halipo tena.”

Dodoma ina mechi tatu ngumu katika viwanja vya ugenini ikianza na Polisi Tanzania inayoonekana kutokuwa na kiwango bora msimu huu na baada ya hapo itakwenda Tanga kucheza dhidi ya Coastal kisha itamalizana na KMC.

Baada ya mechi tatu za ugenini zinazoonekana kuwa mlima mkubwa kwa Dodoma Jiji kutokana na kiwango ilicho nacho itarudi nyumbani kucheza na mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Bara, Yanga.

Chanzo: Mwanaspoti