Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kwa Kelvin john mambo sio shwari

Kelvin John Mbappe Mchezaji kinda wa Kitanzania, Kelvin John

Mon, 9 Oct 2023 Chanzo: Dar24

Mchezaji kinda wa Kitanzania, Kelvin John ameendelea kuandamwa na jinamizi la chama lake la vijana la KRC Genk U23 kuonyeshwa kadi nyekundu kwenye michezo ya ligi ya wachezaji wa akiba huko Ubelgiji ‘Challenger Pro League’.

Jinamizi hilo limeifanya timu hiyo kuendelea kuwa na wakati mgumu kwa kukumbana na vipigo ambavyo vimewafanya kuendelea kushuka kwenye msimamo wa ligi hiyo tofauti na awali na walikuwa katika nafasi za juu.

Katika michezo minane iliyopita ya Challenger Pro League chama la Kelvin tayari limeonyeshwa kadi nne nyekundu katika michezo minne tofauti ikiwemo miwili iliyopita ambayo wamekumbana na jinamizi hilo.

Wakiwa katika nafasi nzuri ya kuibuka na ushindi wikiendi iliyopita dhidi ya Beerschot VA, KRC Genk U23 ilijikuta ikitandikwa mabao 2-1 huku ikiwa pungufu baada ya Ibrahima Bangoura kulimwa kadi nyekundu.

Kelvin alitoa asisti ya bao la chama lake ambalo lipo nafasi ya nane kwenye msimamo wa Challenger Pro League.

Chanzo: Dar24