Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kwa Kazi Simba kuna kazi

Hussein Kazi Kwa Kazi Simba kuna kazi

Wed, 7 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Simba jana ilishinda mabao 4-0 dhidi ya Tabora United kwenye mchezo wa ligi Kuu Bara, huku beki Keneddy Juma akichukua mikoba ya Hussein Kazi kuendelea kufanya kazi ya kuziba bengo la Henock Inonga.

Lakini, kuanza kuingia kwa Kazi ndani ya kikosi cha kazi kuna maana kwamba hivi sasa katika kikosi hicho 'Kazi ameleta kazi' kwa wenzake, hasa kwa Kennedy. 

Twende pamoja. Wakati Simba wakishuka dimbani, beki wao kisiki Henoc Inonga leo ana kibarua cha kucheza mechi ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) dhidi ya wenyeji Ivory Coast Februari 7 ikiwa ni hatua ya nusu fainali na akitoboa tu, basi Mkongomani huyu na chama lake watatinga fainali za mashindano hayo. Kina Inonga wametinga hatua ya nusu fainali baada ya kuifunga Guinea kwa mabao 3-1.

Katika hatua hiyo aliyofikia beki huyo ambaye ni panga pangua kikosi cha kwanza cha Wakongomani hao, tayari amekosa mechi tatu - moja ikiwa ya Kombe la Shirikisho la Azam (ASFC) dhidi ya Tembo FC timu yake ikiibuka na ushindi wa mabao 4-0.

Kakosa pia michezo miwili ya Ligi Kuu Bara - dhidi ya Mashujaa timu yake ikiibuka na ushindi wa bao 1-0 lililofungwa na Said Ntibazonkiza 'Saido', huku nafasi yake ikichukuliwa na Hussein Kazi ambaye tayari amecheza dakika 180 bila kuruhusu bao. Pia kaikosa jana Tabora United ambayo ilichapwa mabao 4-0 na Simba. Hata hivyo, jana Kennedy Juma alianza kikosini sambamba na Che Malone.

Inonga endapo atafanikiwa kuvuka tena hatua ya mshindi wa tatu, basi ataacha pengo Simba ambayo itakuwa na mchezo Februari 9 dhidi ya Azam FC, huku akiwa na kibarua Februari 10 na akitinga fainali pia ataikosa Geita Gold ambayo itachezwa Februari 12 huku yeye akiwa na kibarua Februari 11.

Hivyo ni wazi kuwa Kazi atakuwa na kazi kubwa ya kufanya kwenye eneo la ulinzi akicheza sambamba na Che Malone ambaye alikuwa anacheza sambamba na Inonga katika tarehe hizo ambazo zinagongana na michuano hiyo.

Wakati Baka akimpasua kichwa kocha Abdelhak Benchika tayari amempa nafasi Kazi ambaye ameonyesha utulivu kwenye kikosi akicheza kwa dakika 180 bila kuruhusu ukuta wake kupitisha bao, ingawa jana pia Kennedy alifanya hivyo dhidi ya Tabora United.

KAZI ATOA NENO Akizungumza na Mwanaspoti, Kazi amesema kitendo cha kocha kuendelea kumpa nafasi ya kucheza anamjengea kujiamini na kupata nguvu ya kupambana zaidi ili huduma yake iisaidie timu hiyo.

"Si jambo dogo Simba ina wachezaji wengi. Kocha anapokupa nafasi ya kucheza ina maana anataka ufanye kitu anachoona kinaifaa timu. Kadri ninavyocheza naendelea kujiamini na morali inaongezeka," amesema Kazi.

"Kwenye nafasi yangu kuna wachezaji wenye uzoefu kama Henock Inonga, Che Malone na Kennedy ninapocheza nao kuna vitu najifunza kutoka kwao."

Amesema kocha alianza kumpa nafasi kubwa kwenye Kombe la Mapinduzi na tangu hapo alijikuta akibadilisha mtazamo na kujifunza kuwa na subira pamoja na kuamini kwamba ipo siku atakuwa muhimu kikosini.

Hata hivyo, Kazi bado ana kibarua kizito kwani kwa sasa amejikuta akianzishwa kutokana na kukosekana kwa Inonga aliyepo Afcon.

Kocha Benchikha amekuwa akiwatumia zaidi mabeki Inonga na Che Malone kwenye nafasi ya beki ya kati, huku Kennedy akiingia na kutoka kwenye mechi za Ligi Kuu na hata ya kimataifa, wakati Kazi huwa anaishia benchi au jukwaani.

Lakini kwa kazi kubwa aliyoionyesha kupitia mechi alizopata na kutokuwepo kwa Inonga kikosini kunamfanya Kazi aendelee kukaza kila nafasi anayopewa ili kumshawishi kocha kuendelea kumtumia akila sahani moja na mastaa hao.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live