Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kwa Huyu Sancho bado sana

Jadon Sancho Jadon Sancho

Tue, 6 Dec 2022 Chanzo: Mwanaspoti

Winga wa Manchester United, Jadon Sancho atakosa mazoezi ya kujiweka fiti yanayoendelea huko Hispania kwa sababu bado hajamaliza programu yake maalumu aliyopangiwa na kocha wake, Erik ten Hag.

Wachezaji wa Man United walikwea pipa kwenda Hispania kwa ajili ya mazoezi hayo bila ya winga huyo na watacheza mechi mbili za kirafiki dhidi ya Cadiz utakaochezwa kesho Jumatano, mchezo mwingine utakaofuata utakuwa dhidi ya Real Betis utakaopigwa Desemba 10.

Aidha kwa upande wa Sancho ataendelea na mazoezi peke yake kwani ni sehemu ya programu ambayo itakayomsaidia kujiweka fiti ili arudi kwenye ubora wake, kwahiyo hataungana na wachezaji wenzake Hispania.

Hivi karibuni picha na video za Sancho zilizagaa mitandaoni zikimuonyesha akifanya mazoezi peke yake sambamba na kocha ambaye hakufahamika jina lake.

Aidha kwa mujibu wa ripoti, Kocha Ten Hag alitoa maagizo kwamba Sancho atengewe eneo maalumu kwa ajili ya mazoezi hayo yanayoendelea huko Uholanzi.

Wachezaji wote ambao hawajapata nafasi ya kwenda Qatar walitakiwa kuripoti kwa ajili ya safari ya Hispania akiwemo Alex Telles aliyekuwa akikipiga kwa mkopo Sevila. Jumla ya wachezaji waliosafiri ni 13.

Baadhi ya mastaa wa wazoefu waliomo kwenye safari hiyo ni Davide de Gea, Scott Mctominay, Anthony Martial, Donny van de Beek, Anthony Elanga pamoja na kinda anayekuja kasi kwa sasa Alexandro Gernacho.

Sancho amefunga mabao matatu katika mechi nane alizocheza msimu huu lakini baada ya hapo hakucheka na nyavu tena.

Winga huyo anayelipwa Pauni 350,000 kwa wiki ameshindwa kung’ara Manchester United tangu alipojiunga na timu hiyo akitokea Ligi kuu ya Ujerumani ya Bundesliga katika kikosi cha Borussia Dortmund kwa kitita cha Pauni 73 milioni.

Chanzo: Mwanaspoti