Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kwa Diarra simu zimeanza kuita

Djigui Diarra Maliii Djigui Diarra

Mon, 29 Jan 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Mashabiki wa Yanga wanaisubiri kwa hamu saa 2 usiku ya kesho kushuhudia mastaa wawili wa timu hiyo, Diarra Djigui na kiungo mshambuliaji Stephanie Aziz KI watakawakilisha nchi za Mali na Burkina Faso katika mechi ya 16 Bora ya fainali za Afrika (Afcon) 2023, huku mmojawao akishtua kwa kugombewa Ulaya.

Aziz KI anaiwakilisha Burkina Faso, wakati Diarra akiichezea Mali na ni lazima mmojawao ataaga michuano hiyo kesho zitakapokutana kutegemea matokeo ya dakika za pambano hilo litakalopigwa kwenye Uwanja wa Amadou Gon Coulibaly, jijini Korhogo, lakini mmoja kati ya hao, simu zimeanza kuita tangu wakiwa kambi ya timu hizo.

Ipo hivi. Kipa Diarra ambaye ni kati ya makipa ubora na kutengeneza jina kubwa kwenye fainali hizo za Afcon zinazoendelea Ivory Coast, taarifa za uhakika ni ameanza kupokea ushawishi wa kutimkia mataifa mawili ya Ulaya kama sio Ufaransa basi Ubelgiji.

Kocha wa timu ya taifa ya Mali, Eric Sekou Chelle anayemnoa Diarra amelifichulia Mwanaspoti kambini kwake kuna maskauti kutoka Ulaya wamekuwa wakimuulizia kipa huyo wakitaka kumpeleka Ulaya.

Akizungumza na Mwanaspoti kwa njia ya simu kutoka Ivory Coast, Chelle alisema licha ya kushangazwa kwa Diarra kuikosa tuzo ya kipa bora wa hatua ya makundi, lakini anaamini kipa huyo ndiye alistahili heshima hiyo badala ya kipa wa Guinea ya Ikweta, Jesus Owono aliyetangazwa na Shirikisho la Soka la Afrika (CAF).

Owono kwenye mechi tatu za makundi amefanikiwa kushinda mechi mbili na kutoa sare moja, akiruhusu mabao matatu wakati Diarra akishinda moja na kutoa sare mbili akiruhusu mabao mawili pekee, kitu kilichomshangaza kocha wa Mali.

Hata hivyo, Chelle alisema hatashangaa kuona Diarra akienda kucheza soka Ulaya baada ya maskauti kadhaa kumfuata kambini kipa huyo bora wa mara mbili mfululizo wa Ligi Kuu Bara.

Kocha huyo alisema maskauti hao wanaona kipa huyo anastahili kucheza Ulaya kwa ubora alionao na anaoendelea kuuonyesha akiwa klabuni kwake na hata kwenye fainali hizo.

“Unapochagua kipa bora sidhani kama ni sawa kuangalia timu yake imeshinda mechi ngapi kuliko kuangalia ameruhusu mabao mangapi, mimi binafsi hii tuzo alistahili Djigui (Diarra) tunauangalia mpira unaochezwa wazi,” alisema Chelle na kuongeza;

“Sishangai kila mechi yetu inapokwisha tunawaona maskauti wa Ufaransa na Ubelgiji wakimfuata na kutaka kujua kama watampata wakimpa ofa kubwa tofauti, sawa huo ni uamuzi wake na klabu anayoichezea, lakini huyu ni kipa bora.

Chelle aliongeza ubora mkubwa wa Diarra ni namna anavyojua kuwasiliana na timu yake nzima akiwa uwanjani, pia kuchezesha timu inapoanza kupanga mashambulizi ubora ambao anaweza kucheza klabu zozote kubwa Ulaya.

“Djigui ni bora hata anapokuwa klabuni kwake, unaweza kuona jinsi anavyojua kuanzisha mashambulizi kuanzia nyuma, yuko imara langoni lakini jambo bora zaidi ni kipa ambaye anajua kuipanga timu yake ikacheza kwa kutulia na kukaba kwa akili,” alisema Chelle ambaye anajiandaa kuvaana na Burkina Faso ya Aziz KI katika mechi ya 16 Bora itakayopigwa kesho saa 2:00 usiku.

Chanzo: Mwanaspoti
Related Articles: