Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kwa De Jong! Vita ni nzito EPL

De Jong Frankie Frankie de Jong

Sun, 12 Mar 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Patachimbika. Ndicho unachoweza kusema baada ya Chelsea kudhamiria kuingia vitani na Manchester United katika mchakato wa kunasa saini ya kiungo wa Kidachi, anayekipiga Barcelona, Frenkie de Jong mwishoni mwa msimu huu.

De Jong, 25 alikuwa kwenye mpango wa Man United katika dirisha la majira ya kiangazi la mwaka jana kwa muda mrefu, kabla ya mpango huo kukwama na mchezaji huyo kushindwa kwenda kuungana na kocha wake wa zamani Erik ten Hag huko Old Trafford.

Man United badala yake ilimsajili kiungo wa Real Madrid, Casemiro kwa mkwanja wa Pauni 70 milioni na tangu wakati huo maisha yao ya ndani ya uwanja yamekuwa matamu.

Hata hivyo, katika mipango ya msimu ujao, Man United bado imeonyesha dhamira ya kunasa saini ya De Jong kutokana na kocha Ten Hag kusimamia mpango wake ule wa kunasa huduma ya Mdachi huyo kwenye dirisha lijalo.

Lakini, safari hii imeripotiwa Man United watakuwa kwenye vita kali na Chelsea, kutokana na wababe hao wa Stamford Bridge, nao kuhitaji huduma ya De Jong.

Ripoti zinadai kwamba De Jong atakwenda kufanywa kuwa staa mkubwa kwenye kikosi cha Graham Potter kwa ajili ya msimu ujao wa 2023-24 huku bosi wa timu hiyo akilenga kutumia Pauni 71 milioni kwenye kunasa saini yake.

Mmiliki mwenza wa Chelsea, bilionea Todd Boehly tayari ameshatumia Pauni 600 milioni kwenye usajili wa mastaa wapya katika madirisha mawili tu yaliyopita, hivyo si mtu anayefikiria sana katika kufungua pochi kunasa mastaa wapya.

Chelsea inahitaji nguvu mpya kwenye sehemu ya kiungo baada ya Mason Mount na N'Golo Kante hatima zao kutofahamika vyema huku wakiwa hawafahamu pia kama watamchukua jumla kiungo Denis Zakaria anayecheza kwa mkopo kutoka Juventus. Tangu alipotua Barca akitokea Ajax, Julai 2019, De Jong amefunga mabao 15 na kuasisti mara 19 katika mechi 172 za michuano yote aliyochezea miamba hiyo ya Nou Camp kwenye sehemu ya kiungo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live