Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kwa Allasane Diao Azam, ishu ni Dube

Allasane Diao I.jpeg Kwa Allasane Diao Azam, ishu ni Dube

Sat, 16 Sep 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Azam FC imeendelea kujifua ili kuhakikisha inatwaa ubingwa wa Ligi Kuu Bara msimu huu na juzi ilicheza mechi ya kirafiki na kuichapa Mbuni iliyopo Championship, huku washambuliaji Prince Dube na Alassane Diao wakimnyima usingizi kocha mkuu wa chama hilo, Youssouph Dabo.

Dabo alisema Allasane amekuwa akipata ugumu kumtumia kwa vile Dube yupo moto tofauti na wakati anajiunga na timu hiyo, hivyo anampa wakati mgumu kuamua amtumie nani nafasi ya mshambuliaji wa kati kutokana na kuwa ni eneo ambalo wawili hao wanacheza.

“Tuna washambuliaji zaidi ya watatu wakiwemo Dube na Allasane, wote wako kwenye kiwango bora jambo tunalojivunia lakini tunataka kila mmoja acheze ndio maana kuna baadhi ya mechi mnaona tunawabadili maeneo,” alisema Dabo aliyemsajili Allasane mwanzo wa msimu.

Kocha huyo alisema Dube kwa sasa yupo kwenye ubora akiwa ni miongoni mwa wachezaji wanaotengeneza msingi wa Azam na kuweka wazi maandalizi yao yalivyokuwa kabla ya kuivaa Singida Fountain Gate Septemba 21.

“Muda tuliokaa bila mechi za mashindano tulikuwa na programu mbalimbali na tumezifanya vizuri,” Washambualiaji wengine wa Azam wanaocheza eneo la ushambuliaji ni Idriss Mbombo na Abdul Seleman ‘Sopu’ ambao wote wako moto. Dube amefunga mara saba msimu huu.

Chanzo: Mwanaspoti