Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kuziona Yanga, Geita Kirumba buku tano tu!

Yanga Mbeya Ihefuu Kuziona Yanga, Geita Kirumba buku tano tu!

Thu, 5 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Bado saa 24 tu kabla ya Geita Gold kuikaribisha Yanga kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, jijini hapa katika pambano la Ligi Kuu Bara, huku wenyeji wakiweka viingilio vitakavyowaruhusu mashabiki wengi kulicheki pambano hilo litakaloanza kuanzia saa 10:00 jioni.

Mashabiki wa soka wa jijini Mwanza na mikoa ya jirani ya Kanda ya Ziwa, watalazimika kulipa Sh 5,000 kwa mzungumzo na vile vingine vikiwa ni kati ya Sh 10,000 na Sh 20,000 kwenye majukwaa ya VIP A na B.

Akizungumza jana Jumatano Oktoba 4 jijini hapa katika mkutano wake na waandishi wa habari kuhusu maandalizi ya mchezo huo, Mkurugenzi wa Mashindano wa Geita Gold, Liberatus Pastory ameipongeza bodi ya Ligi kwa kuurejesha nyuma mchezo kutoka Oktoba 22 kwani itawasaidia timu yao kuwa fiti kuliko ambavyo wangekaa muda mrefu bila kucheza mchezo wowote tangu walipocheza Septemba 30 dhidi ya KMC.

"Wananchi wa Mwanza na mikoa jirani tunawakaribisha kwenye mchezo huu sisi tumejipanga kufanya vizuri kwenye mchezo huo na viingilio vyetu ni rafiki Sh20,000 VIP A, Sh10,000 VIP B na Sh5,000 mzunguko,"

"Mwanza ni nyumbani hatuchezi ugenini, Watu wa hapa waipokee Geita watupe sapoti kama siku zote," amesema Pastory

Mkurugenzi wa Mashindano na Ufundi wa Chama cha Soka Mkoa wa Mwanza (MZFA), Khalid Bitebo amesema maandalizi ya mchezo huo yamekamilika, ambapo ili kuondoa foleni zisizo za lazima wamekubaliana na menej wa uwanja huo kufungua milango kuanzia saa 4 asubuhi.

Bitebo amesema tiketi zote zitauzwa kwa njia ya elektroniki na tayari vituo vitakavyouza tiketi hizo vimewekwa wazi ambavyo ni uwanja wa Nyamagana, ofisi za TTCL, Buhongwa, Nyegezi, Buzuruga, Pasiansi na nje ya uwanja wa CCM Kirumba.

"Tumekutana na meneja wa uwanja maandalizi yanaendelea na yamefikia asilimia 70 leo wameanza kuufyeka na ametuhakikishia watafungua milango yote tisa, kwahiyo mashabiki kutoka sehemu mbalimbali wajitokeze kwa wingi siku hiyo," amesema Bitebo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: