Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kuziona Yanga, Azam buku tano

Kiingilio Pic Data (600 X 308) Mchezo wa Yanga vs Azam jumapili hii

Tue, 26 Oct 2021 Chanzo: Mwanaspoti

Msemaji wa Yanga, Haji Manara amesema kuwa kiingilio cha chini katika mchezo wao wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Azam FC ni shilingi elfu tano (5000).

Timu hizo zinakutana Jumamosi katika mechi ya Ligi Kuu Bara mchezo utakaochezwa kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.

Akitaja viingilio vya mchezo huo Manara amesema viingilio kwenye viti vya mzunguko ni elfu tano, VIP B na C ni 10,000 wakati kwa upande wa VIP A ni shilingi elfu 15,000.

Akizungumza hali ya kikosi chao kuelekea mchezo huo Manara amesema mchezaji pekee atakayekosekana ni Dickson Ambundo ila waliobaki wote wako tayari kwa ajili ya mchezo huo muhimu.

"Tumewaangalia Azam kwenye mechi yao na Pyramids ni timu nzuri yenye wachezaji wenye ari ya kupambana na walioimarika ila dhamira yetu kama Klabu msimu huu ni kutwaa ubingwa," amesema. Advertisement

Manara ameongeza kuwa kutakuwa na wasanii watakaotumbuiza katika mchezo huo na kuanzia muda wowote kuanzia sasa watawatangaza rasmi.

"Mchezo wa mpira wa miguu ni mtoko na sisi tunalijua hilo hivyo hatutaki mashabiki waje uwanjani halafu waboreke bali watakutana na burudani mbalimbali ambazo tutaziandaa kwa ajili yao," amesema.

Yanga inashuka uwanjani ikiwa na alama tisa kwenye nafasi ya pili wakati Azam FC ikikusanya alama nne ikiwa kwenye nafasi ya 10.

Chanzo: Mwanaspoti